Frank Domayo aliivaa 'nje ndani' jezi ya Simba, kwa sababu gani sasa? |
Katika mchezo huo, Simba SC ilishinda mabao 3-1, baadhi ya wachezaji walivalia jezi za wapinzani bila woga, lakini wengine walivaa ‘kiwoga woga’.
Malinzi akimvalisha Medali Mkude kulia akiwa amevalia jezi ya Yanga SC |
Mkude aliivua jezi hiyo ya Yanga wakati anaondoka uwanjani |
Miongoni mwa waliovaa jezi za wapinzani kiwoga woga ni kiungo wa Yanga, Frank Domayo ambaye aliigeuza jezi hiyo ‘nje ndani’. Hii ilimaanisha nini, yeye Yanga sana, alikerwa na kipigo hadi akachukia jezi ya wapinzani, au alihofia mashabiki tu.
Uvaaji wa jezi ya wapinzani wa Domayo ulikuwa tofauti sana na kiungo mwenzake, Jonas Mkude wa Simba SC ambaye aliivaa bila woga jezi ya Yanga SC na kwa kujiamini.
Mkude alikwenda na jezi hiyo ya Yanga SC kuchukulia hadi Medali yake ya Dhahabu kwa mgeni rasmi, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya ushindi na akapiga nayo picha katika sherehe za kukabidhiwa Kombe.
Baada ya hapo, aliivua akaenda kupanda basi na bila shaka amekwenda kuiweka nyumbani kwake kama kumbukumbu.
0 comments:
Post a Comment