BAO la dakika ya 66 la Edin Dzeko limeipa Manchester City ushindi wa 1-0 dhidi ya Crystal Palace na kupanda kileleni mwa Ligi Kuu ya England jioni hii.
Hilo ni bao la 50 kwa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Bosnia tangu ajiunge na Manchester City, ambalo linaipa timu yake ushindi wa 10 mfululizo Uwanja wa nyumbani, Etihad.
Man City sasa imetimiza pointi 41, baada ya kucheza mechi 19 na kusimama kileleni mwa Ligi Kuu England, ikiipiku Arsenal inayobaki na pointi zake 39, ingawa imecheza mechi 18.
Kiulaini anatumbukiza: Mshambuliaji wa Manchester City, Edin Dzeko akimtungua kipa Julian Speroni kuipa timu yake ushindi wa 1-0 dhidi ya Crystal Palace
Dzeko (kulia) akishangilia baada ya kufunga
Dzeko akipongezwa na wenzake, Alvaro Negredo (kushoto) baada ya kufunga bao pekee Uwanja wa Etihad
Katika mchezo mwingine, bao pekee la Danny Welbeck dakika ya 57 limeipa Manchester United ushindi wa 1-0 pia dhidi ya Norwich ugenini.
Ushindi huo, unaifanya United ifikishe pointi 34 baada ya kucheza mechi 19 na kubaki nafasi ya sita, nyuma ya Everton yenye poinyi 36 pia, Liverpool pointi 36 na Chelsea 37.
Shujaa! Danny Welbeck akishangilia bao lake pekee aliloifungia Manchester United leo
0 comments:
Post a Comment