// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); CHELSEA YAIKALISHA LIVERPOOL DARAJANI, SUAREZ AFANYIWA 'UNDAVA' KINOMA, SPURS NAYO YAUA 3-0 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE CHELSEA YAIKALISHA LIVERPOOL DARAJANI, SUAREZ AFANYIWA 'UNDAVA' KINOMA, SPURS NAYO YAUA 3-0 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, December 29, 2013

    CHELSEA YAIKALISHA LIVERPOOL DARAJANI, SUAREZ AFANYIWA 'UNDAVA' KINOMA, SPURS NAYO YAUA 3-0

    KOCHA Mreno Jose Mourinho ametoka na furaha Uwanja wa Stamford Bridge jioni hii, baada ya timu yake, Chelsea kuilaza mabao 2-1 Liverpool katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
    Shukrani kwake mshambuliaji mkongwe, Samuel Eto'o aliyefunga bao la ushindi dakika ya 34 akimalizia pasi ya Oscar ndani ya sita.
    Mabeki wa Chelsea walimchezea 'kindava' mshambuliaji Luis Suarez na akatoka uwanjani bila kufunga bao.
    Shujaa; Samuel Eto'o akishangilia baada ya kufunga bao la ushindi, Chelsea ikiilaza Liverpool 2-1

    Liverpool ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya nne, mfungaji Skrtel, lakini Edin Hazard akasawazisha dakika ya 17.
    Kwa ushindi huo, Chelsea inatimiza pointi 37 na kubaki nafasi ya tatu, wakati Liverpool inabaki na pointi zake 36.
    Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo leo, Tottenham Hotspur imeifunga Stoke City mabao 3-0, wafungaji Soldado dakika ya 37, Dembele dakika ya 65 na Lennon dakika ya 69. 
    Ushindi raha; Lennon kulia akishangilia Adebayor baada ya kuifungia Spurs katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Stoke leo
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CHELSEA YAIKALISHA LIVERPOOL DARAJANI, SUAREZ AFANYIWA 'UNDAVA' KINOMA, SPURS NAYO YAUA 3-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top