Na Mahmoud Zubeiry, Chamazi
KIKOSI kizima cha Azam FC, kinatarajiwa kuondoka Dar es Salaam Januari 1, kuelekea visiwani Zanzibar kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi.
Meneja wa Azam FC, Jemadari Said Kazumari ameiambia BIN ZUBEIRY kwamba, Azam itaondoka na wachezaji 33 wakiwemo waliopandishwa kutoka akademi ya timu hiyo.
Hata hivyo, katika kikosi hicho kiungo Mkenya, Humphrey Mieno anaweza kukosekana kutokana na kutowasili hadi sasa kujiunga na wenzake mazoezini.
Jemadari alisema Mieno baada ya kupewa ruhusa ya awali hakurejea muda wake ulipomalizika na uongozi ulipowasiliana naye akasema ana matatizo ya kifamilia, hivyo akaongezewa muda ambao pia umeisha.
MSAFARA WA AZAM ZANZIBAR
WACHEZAJI;
AISHI SALLUM MANULA
ABDALLAH SEIF KARIHE.
AGGREY MORIS AMBROSI
BRAISON RAFAEL NKULULA
BRIAN UMOMY
DAVID JOHN MWANTIKA
ERASTO EDWARD NYONI
FARID MUSSA SHAH
GAUDENCE EXAVERY MWAIKIMBA
GADIEL MICHAEL MBAGA
HIMID MAO MKAMI
IBRAHIM JOEL MWAIPOPO
ISAMEL ADAM GAMBO
JABIR AZIZ STIMA
JOHN RAFAEL BOCCO
JOSEPH LUBASHA KIMWAGA
KELVIN FRIDAY IDD
KIPRE HERMANN BRICE TCHETCHE
KONE ISMAEL MOUHAMED
KHAMIS MCHA KHAMIS
LUCKSON JONATHAN KAKOLAKI
BOLOU WIFRED MICHAEL KIPRE
MALIKA PHILIPO NDEULE
MUDATHIR YAHYA ABBASI
MWADINI ALI MWADINI
REYNA ELIMINIUS MGUNGILA
SAID HUSSEIN MORADI
SAMIH ALI NUHU
SWALEHE ABDALLAH
WANDWI JACKSON WANDWI
WAZIRI SALLUM OMAR
SALLUM ABUBAKAR SALLUM
HUMPHREY OCHIENG MIENO
HAMADI JUMA HAMADI
VIONGOZI.
JOSEPH MARIUS OMOG
KALIMANGONGA SAM DANIEL ONGALA
IBRAHIM SHIKANDA CHIMWAGA
IDD ABUBAKAR MWICHUMU
VIVEK NAGUL
MWANANDI JUMA MWANKEMWA
VICENT JUMA MADEGE
TWALIBU MBARAKA
YUSUF DAVID NZAWILA
SWALEHE JUMAPILI AWADHI
JEMEDARI SAID KAZUMARI
“Na bado tumekuwa tukimtumia ujumbe wa barua pepe na sms kumuuliza kulikoni amechelewa, lakini bado amekuwa hajibu, hivyo hatuelewi nini kimemkwamisha,”alisema.
Aidha, Jemadari alisema wana mchezaji mpya mazoezini kutoka Don Bosco ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Djunes Kayanda aliyewahi pia kuchezea Zanaco ya Zambia.
Jemadari amesema mshambuliaji huyo wa pili ni kijana mdogo wa umri wa miaka 19 na ingawa kwa sasa hawezi kusajiliwa, lakini uongozi umeamua kumpa muda zaidi kuendelea kumtazama.
Tayari Azam ina wachezaji watano wa kigeni, ambao ni kiungo Kipre Michael Balou na washambuliaji Kipre Herman Tchetche na Muamad Ismael Kone wote kutoka Ivory Coast pamoja na Mganda Brian Umony na Mkenya Mieno.
Kone amesajiliwa msimu huu akichukua nafasi ya beki Mkenya, Joackins Atudo aliyetemwa baada ya kumaliza Mkataba wake.
Azam FC hivi sasa ipo chini ya kocha mpya, Joseph Marius Omog raia wa Cameroon ambaye mara ya mwisho alikuwa kocha wa klabu ya FC Leopard ya Kongo Brazzaville.
Azam jana ilicheza mechi ya kwanza chini ya Omog na kushinda mabao 3-0 dhidi ya Ruvu Shooting ya Pwani katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam jioni hii.
Hadi mapumziko, tayari Azam FC, walio chini ya kocha mpya Mcameroon, Joseph Marius Omog walikuwa mbele kwa mabao 2-0.
John Raphael Bocco alitangulia kuifungia Azam bao la kwanza dakika ya 10 kazi nzuri Mganda, Brian Umony ambaye anaonekana kurudi katika kasi yake ya mchezo baada ya kuandamwa na majeruhi msimu uliopita.
Bao la pili liliwekwa nyavuni kwa mkwaju wa penalti na mshambuliaji wa Ivory Coast, Kipre Herman Tchetche dakika ya 30, baada ya Ayoub Kitala kuurudisha kwa mkono mpira uliokuwa unaelekea nyavuni.
Refa Israel Mujuni Nkongo alimpa kadi nyekundu beki wa Ruvu na kuifanya timu ya Charles Boniface Mkwasa ‘Master’ imalizie dakika 50 za pambano hilo ikiwa pungufu.
Mchezo ulikuwa mzuri kipindi cha kwanza timu zote zikicheza soka ya kufundishwa na makocha waliosomea Ujerumani, Mkwasa wa Ruvu na Omog wa Azam FC.
Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko karibu ya vikosi vizima na aliyekuwa kivutio katika ngwe hiyo ni mshambuliaji mpya kutoka Ivory Coast Muamad Ismael Kone aliyeingia pia kwa upande wa Azam.
0 comments:
Post a Comment