// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); TFF YAMTAMBUA RAGE BADO MWENYEKITI SIMBA, YAMTAKA AITISHE MKUTANO NDANI YA SIKU 14 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE TFF YAMTAMBUA RAGE BADO MWENYEKITI SIMBA, YAMTAKA AITISHE MKUTANO NDANI YA SIKU 14 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

        Saturday, November 23, 2013

        TFF YAMTAMBUA RAGE BADO MWENYEKITI SIMBA, YAMTAKA AITISHE MKUTANO NDANI YA SIKU 14


        Na Boniface Wambura, Ilala
        MWENYEKITI wa Simba, Ismail Aden Rage ameagizwa kuitisha Mkutano Mkuu wa Dharura wa klabu ndani ya siku 14 kuanzia sasa.
        Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa agizo hilo baada ya kubaini kuwa mgogoro katika klabu baada ya kupokea barua mbili; moja kutoka Kamati ya Utendaji ikielezea kumsimamisha uongozi Rage, na nyingine kutoka kwa Mwenyekiti huyo ikielezea kutotambua kusimamishwa huko.
        TFF bado inamtambua Rage

        Uamuzi wa TFF umefanywa kwa kuzingatia Ibara ya 1(6) ya Katiba ya Simba inayosema: “Simba Sports Club ni mwanachama wa TFF, itaheshimu Katiba, kanuni, maagizo na uamuzi wa TFF na FIFA, na kuhakikisha kuwa zinaheshimiwa na wanachama wake.”
        TFF itatuma wawakilishi wake katika mkutano huo, na kumuagiza Mwenyekiti wa Simba kuhakikisha wanachama wote wenye hoja wanapata fursa ya kusikilizwa.
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: TFF YAMTAMBUA RAGE BADO MWENYEKITI SIMBA, YAMTAKA AITISHE MKUTANO NDANI YA SIKU 14 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry