Na Ezekiel Kamwaga, Msimbazi
KUFUATIA matukio yaliyotokea katika pambano la jana, Alhamisi, Oktoba 31, 2013 dhidi ya Kagera Sugar kwenye Ligi Kuu ya Tanzania, klabu ya Simba inapenda kutoa maelezo yafuatayo.
Mosi, Simba SC inalalamikia uchezeshaji mbovu wa mwamuzi, Mohamed Theofilo kutoka mkoani Morogoro ambaye ndiye aliyekuwa mwamuzi wa kati katika mechi ya jana.
Kwa bahati nzuri, baadhi ya vyombo vya habari vya hapa nchini tayari vimeandika kwamba mwamuzi huyo hakumudu mchezo wa jana na hivyo maelezo haya ya klabu hayatokani na uchungu wa kupoteza pointi mbili muhimu bali ni ukweli wa wazi.
Mara zote klabu ya Simba imekuwa ikisisitiza umuhimu wa waamuzi kufuata Sheria zote 17 zinazotawala mchezo huu. Katika pambano la jana, adhabu ya penalti aliyoitoa mwamuzi haikuwa halali na ilitolewa katika wakati ambapo muda wa kuchezwa mechi hiyo ulikuwa umemalizika.
Mchezaji aliyedaiwa kufanyiwa madhambi aliushika mpira akiwa nje ya eneo la penalti na alijirusha mwenyewe (diving) kwenda kwenye eneo la hatari. Mwamuzi msaidizi ambaye alikuwa jirani na tukio hakuonyesha bendera kuashiria madhambi yoyote yaliyofanyika lakini cha ajabu, Theofilo ambaye alikuwa umbali wa zaidi ya mita 30 kutoka eneo la tukio, ndiye aliyeona madhambi na kuamuru penalti.
Penalti hiyo ilitolewa katika dakika ya tano na nusu wakati muda uliokuwa umeongezwa ulikuwa dakika nne tu. Hii inajenga mazingira kwamba mwamuzi alikuwa anatafuta fursa ya kuihujumu Simba.
Baadhi ya vyombo vya habari na washabiki walieleza pia kushangazwa na uamuzi mbaya dhidi ya Simba wakati wa mechi kati ya Simba na Azam. Maonevu haya ya wazi dhidi ya Wekundu wa Msimbazi yameanza kuutia wasiwasi uongozi, wachezaji na washabiki wa klabu.
Kupitia taarifa hii, tunaomba vyombo husika vimchunguze mwamuzi huyu na kuangalia uchezeshaji wake na hatimaye achukuliwe hatua zinazostahili.
Kwa taarifa hii, tunamwomba Rais mpya wa TFF, Jamal Malinzi, aangalie namna bora ya kuboresha viwango vya waamuzi wa Tanzania kwani kwa sasa wengi wanatia aibu na ndiyo maana taifa letu sasa limeshindwa kutoa waamuzi kwenda kwenye mashindano au mechi kubwa za kimataifa.
Klabu ya Simba inasisitiza kwamba haitamuonea mwamuzi ambaye ametimiza wajibu wake lakini haitasita kumshutumu au kusema ukweli bila kupindisha pale ambapo uamuzi mbovu unaathiri matokeo ya mechi.
KUHUSU FUJO ZILIZOTOKEA
Kwa niaba ya uongozi wa Simba, Mwenyekiti wa Simba, Mhe; Ismail Aden Rage, anapenda kuomba radhi kwa TFF, Serikali, uongozi wa Uwanja wa Taifa na wadau wa soka kutokana na vitendo vya uvunjifu wa amani na uharibifu wa mali vilivyofanywa na baadhi ya washabiki wa Simba katika pambano la jana.
Rage alisema fujo za jana zilimshtua hata yeye kwa vile wapenzi wa Simba, kwa tabia, hawapendi vurugu na wamekuwa na utaratibu wa kawaida wa kuwapigia makofi wachezaji hata pale timu inapofungwa.
Kilichotokea jana, kwa mujibu wa Rage, ni jambo la aina yake na linalotakiwa kufanyiwa tafakari jadidi kubaini nini haswa kilikuwa chanzo na muktadha wa yaliyotokea.
Hata hivyo, amesisitiza Rage, hakuna maelezo yoyote yanayoweza kutolewa kutetea sababu za uharibifu wa mali na uvunjifu wa amani uliotokea na ametoa wito kwa wana Simba kujiepusha na kufanya vitendo kama hivyo katika siku za usoni.
Uongozi wa Simba uko tayari kutoa ushirikiano wowote utakaohitajika kwa lengo la kuhakikisha kwamba fujo katika viwanja vya soka zinakomeshwa ili watu wazidi kwenda viwanjani badala ya kubaki majumbani wakihofia vurugu.
TIMU
Wachezaji wa Simba wamepewa mapumziko ya siku mbili mara baada ya mechi ya jana na wanatarajiwa kuingia kambini Jumatatu ijayo kujiandaa na mechi ya Jumatano ijayo dhidi ya Ashanti United itakayopigwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kipa wa Simba SC, Abbel Dhaira akizungumza na refa, Mohamed Theofile anayesindikizwa na Polisi |

0 comments:
Post a Comment