Tumewasoma, hawatishi; Suleiman Kassim 'Selembe' amesema hawazihofii Kenya na Ethiopia |
KIUNGO wa Zanzibar, Suleiman Kassim ‘Selembe’ amesema kwamba wamewaona wapinzani wao wengine katika Kundi A, Kenya na Ethiopia na pamoja na kuwasifu ni wazuri, lakini amesema hawawatishi hata kidogo.
Zanzibar ilianza vyema michuano ya CECAFA Challenge jana kwa kuifunga Sudan Kusini 2-1 Uwanja wa Nyayo na baada ya hapo wachezaji wake wakapanda jukwaani kutazama mechi nyingine ya Kundi hilo kati ya Ethiopia na wenyeji Kenya iliyomalizika kwa sare ya bila kufungana.
Wachezaji wa Zanzibar wakitazama mechi kati ya Ken na Ethiopia jana jana. |
“Sisi baada ya mechi yetu tulipanda jukwaani kutazama mechi ya Kenya na Ethiopia kwa kuwa hao ndiyo wapinzani wetu wajao. Kwa kweli niseme tu timu zote nzuri, lakini sisi hazitutishi, tutapambana nazo ili tuzifunge na kuingia Robo Fainali,”alisema kiungo huyo wa Coastal Union ya Tanga.
Kuhusu mechi ya jana, Selembe alisema kwamba wangeweza kushinda mabao mengi kama si kupoteza nafasi nyingi walizotengeneza.
Khamis Mcha 'Vialli' akisikitika jana baada ya kukosa bao la wazi |
“Na pia ilionekana wakati fulani kama tumezidiwa ni kwa sababu tu ya uchovu wa safari na hali ya hewa ya huku (baridi), lakini tunatarajia kuanzia mchezo ujao tutacheza ile soka yetu haswa ambayo watu wanaifahamu,”alisema.
Zanzibar itashuka tena dimbani Novemba 30 kumenyana na Ethiopia kabla ya kukamilisha mechi zake za kundi hilo kwa kumenyana na Kenya Desemba 3.
0 comments:
Post a Comment