Na Mahmoud Zubeiry Nairobi
KOCHA wa Bara, Kilimanjaro Stars Mdenmark Kim Poulsen amesema kwamba anatarajia kufanya vizuri katika mechi zijazo za Kundi B Kombe la Mataifa ya Afrika Mashatiki na Kati, CECAFA Challenge baada ya sare ya jana ya 1-1 na Zambia.
Stars jana ilitoka nyuma kwa 1-0 hadi mapumziko na kupata sare ya 1-1 kipindi cha pili kwa bao la beki Said Morad, Uwanja wa Kenyatta, Machakos.
Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya mechi, Poulsen alisema mchezo wa jana ulikuwa mkali na ulizikutanisha timu nzuri.
“Kipindi cha kwanza tulicheza mchezo tofauti. Tulitumia sana mipira mirefu na ya juu, ambayo siyo staili yetu ya uchezaji.
“Tulibadilika kipindi cha pili na kuwa bora, tuliwashambulia sana Zambia, tulitengeneza nafasi na kupata bao la kusawazisha. Mrisho Ngassa akakosa bao la wazi sana,”alisema Kim.
Hata hivyo, Kim alisema kwamba baada ya mchezo wa jana anakwenda kufanyia kazi mapungufu ili waweze kushinda mechi zijazo dhidi ya Burundi na Somalia.

Kim Poulsen amesema atafanyia kazi mapungufu timu ifanye vizuri mechi zijazo |
Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya mechi, Poulsen alisema mchezo wa jana ulikuwa mkali na ulizikutanisha timu nzuri.
“Kipindi cha kwanza tulicheza mchezo tofauti. Tulitumia sana mipira mirefu na ya juu, ambayo siyo staili yetu ya uchezaji.
“Tulibadilika kipindi cha pili na kuwa bora, tuliwashambulia sana Zambia, tulitengeneza nafasi na kupata bao la kusawazisha. Mrisho Ngassa akakosa bao la wazi sana,”alisema Kim.
Hata hivyo, Kim alisema kwamba baada ya mchezo wa jana anakwenda kufanyia kazi mapungufu ili waweze kushinda mechi zijazo dhidi ya Burundi na Somalia.
0 comments:
Post a Comment