// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KIIZA NA NIYONZMA WAONYESHANA KAZI MACHAKOS - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KIIZA NA NIYONZMA WAONYESHANA KAZI MACHAKOS - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, November 29, 2013

    KIIZA NA NIYONZMA WAONYESHANA KAZI MACHAKOS

    Na Mahmoud Zubeiry Nairobi
    WACHEZAJI wawili wa Yanga SC, kiungo Haruna Niyonzima na mshambuliaji Hamisi Kiiz leo wanatarajiwa kuonyeshana kazi Uwanja wa Kenyatta, Machakos, Kenya.
    Hiyo ni katika mchezo wa Kundi C wa Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge baina ya timu zao, Uganda ya Kiiza na Rwanda na Niyonzima.
    Hamisi Kiiza ataiongoza Uganda dhidi ya Rwanda leo na chini ni Haruna Niyonzima wa Rwanda

    Mchezo huo utafanyika jioni na utatanguliwa na mchezo mwingine wa kundi hilo kati ya Sudan na Eritrea.
    Kiiza na Niyinzima wamekuwa wakifurahia mafanikio pamoja katika klabu ya Yanga, lakini leo watatengeneza tofauti kwa dakika 90 Uwanja wa Machakos kila mmoja kwa maslahi ya taifa lake.
    Raundi ya kwanza ya CECAFA Challenge inatarajiwa kukamilika leo kwa mechi hizo za Kundi C, baada ya juzi na jana kuchezwa mechi za Kundi A na B. je, ni Kiiza au Niyonzima ataipa ushindi timu yake leo? Bila shaka hilo ni jambo la kusubiri na kuona.   

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIIZA NA NIYONZMA WAONYESHANA KAZI MACHAKOS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top