// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KIIZA ASHINDWA KUMKATA TAMBWE LEO…AKOSA MABAO HAYO HUWEZI KUAMINI KAMA NI DIEGO! - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KIIZA ASHINDWA KUMKATA TAMBWE LEO…AKOSA MABAO HAYO HUWEZI KUAMINI KAMA NI DIEGO! - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, November 01, 2013

    KIIZA ASHINDWA KUMKATA TAMBWE LEO…AKOSA MABAO HAYO HUWEZI KUAMINI KAMA NI DIEGO!

    Na Princess Asia, Dar es Salaam
    HAMISI Friday Kiiza ‘Diego’ wa Yanga SC leo ameshindwa kumkamata mshambuliaji wa Simba SC, Amisi Tambwe anayeongoza kwa mabao katika chati ya wafungaji wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Kiiza leo alipata nafasi kadhaa za kufunga Yanga ikishinda 4-0 dhidi ya JKT Ruvu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam akashindwa kuzitumia, lakini ambayo atalala akiiota ni ya dakika ya 70 alipotengewa mpira ndani ya sita na Simon Msuva, lakini akapiga nje. 
    KInara wa mabao' Amisi Tambwe anaongoza kwa mabao yake tisa

    Kiiza sasa anabaki na mabao yake nane, wakati mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Tambwe jana alifunga moja katika sare ya 1-1 na Kagera Sugar, anapanda kileleni.
    Mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Uganda, The Cranes anafuatiwa na mshambuliaji chipukizi wa kimataifa wa Tanzania, Juma Luizio wa Mtibwa Sugar ambaye pia ana mabao saba.
    Wanaofuatia ni mfungaji bora wa msimu uliopita, Kipre Tchetche wa Azam FC mwenye mabao sita sawa na Elias Maguri wa Ruvu Shooting na Themi Felix wa Kagera Sugar, wakati Mrisho Ngassa wa Yanga ana mabao matano sawa Tumba Swedi wa Ashanti.
    Umekosa sana mabao leo; Hamisi Kiiza akizungumza na Mwenyekiti wa kamati ya Mashindano ya Yanga, Abdallah Bin Kleb kulia


    WANAOONGOZA KWA MABAO LIGI KUU:
    JINA TIMU MABAO
    Amisi Tambwe Simba SC 9
    Hamisi Kiiza Yanga SC 8
    Juma Luizio Mtibwa 7
    Kipre Tchetche Azam FC 6
    Elias Maguri Ruvu Shoot 6
    Themi Felix Kagera 6
    Mrisho Ngassa Yanga SC 5
    Tumba Swedi Ashanti 5
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIIZA ASHINDWA KUMKATA TAMBWE LEO…AKOSA MABAO HAYO HUWEZI KUAMINI KAMA NI DIEGO! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top