KIUNGO Mesut Ozil amekuwa akiteka vichwa vya habari tangu atue Arsenal kwa dau la Pauni Milioni 42.5 kutoka Real Madrid, lakini anaonekana kuekwa akili mno na mpenzi wake, mlimbwende Mandy Capristo.
Nyota huyo wa Ujerumani aliyeisaidia Arsenal kurejesha makali yake katika Ligi Kuu England tangu atue Emirates msimu huu, alipigwa picha akimpiga picha nyota huyo sa Pop mjini London.
Capristo, mwenye umri wa miaka 23, ni bonge la supa staa nchini kwao Ujerumani na kwa sasa ni msanii wa kujitegemea baada ya kujitoa katika bendi ya wasichana wenzake, Monrose, lakini Ozil hawezi kuimba mbele ya watu.
Sema chizzz! Capristo akipozi kupigwa picha na Ozil ambaye alionekana kufurahia kufanya barabarani Jijni London
Mara tu baada ya kuwasili, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 aliweza kuzoeana haraka na wachezaji wenzake.
Ozil alilazimishwa kusimama kwenye kiti mbele ya wachezaji wenzake kuimba, lakini hakufurahishwa sana na hilo.
Alisema: "Sitaki kufanya hivi tena. Sauti yangu si ya kuimba. MimiI si mshiriki wa X Factor kwa na,na yoyote. Ulikuwa ni wimbo wa Kituruki, kitu fulani binafsi niliimba kwa wachezaji wenzangu na ninataka ibaki hivyo. Kwa sababu watu hawakuelewa nilikuwa ninaimba nini, lakini walinishgilia ile mbaya, ambayo nafikiri ni babu kuibwa.'
Unywele wa kimwana: Ozil na Capristo wakirejea ndani baada ya kumaliza kupigana picha
Arsenal inamenyana na Liverpool Jumamosi hii ambayo ikiwa na kikosi chake kamili wakiwemo wapachika mabao hatari, Daniel Sturridge na Luis Suarez wamewasili Emirates.
Lakini mshambuliaji Olivier Giroud amewashukuru Ozil na wachezaji wengine wanaomtengenezea nafasi za kufunga hadi mchezaji wa nne kwa kufunga mabao mengi katika ligi msimu huu hadi sasa.
Mshambuliaji huyo wa kati wa Ufaransa, amefunga mabao nane hadi sasa, lakini pia ametoa pasi nne za mabao ambayo tayari ni zaidi ya mwaka jaan.
Risasi ya Bunduki: Ozil - akiwa mazoezini Ijumaa (kulia) ametua na moto kutoka Hispania
Mastaa wapendanao: Capristo ni maarufu Ujerumani baada kung'ara na bendi ya wasichana kabla ya kuamua kuwa msanii wa kujitegemea
0 comments:
Post a Comment