WINGA Gareth Bale amesema kwamba kwa sasa yuko fiti kabisa baada ya mwanzo mgumu katika kabu yake mpya, Real Madrid na sasa yuko tayari kufanya kuwafanyia mambo mazuri vigogo hao wa Hispania.
Miezi miwili ya mwanzo ya nyota huyo wa Wales ilikuwa migumu Hispania tangu asajiliwe kutoka Tottenham ya England Septemba 1 kutokana na kuandamwa na majeruhi.
Bale aliumia mara mbili katika mwezi wake wa kwanza, lakini ameweza kufunga mabao matatu hadi sasa na kusababisha mabao matano kwa Los Blancos, ambayo inashika nafasi ya tatu kwa ssa katika La Liga na kuongoza kundi lake katika Ligi ya Mabingwa.
Ametulia: Gareth Bale amesema kwa sasa anajisikia yuko vizuri Real Madrid na sasa ni wakati wa kufunga mabao
Bale akijaribu kiat chake kipya cha Adidas Samba Pack kufanyia mazoezi
Bale akifanya mazoezi ya kuwa fiti zaidi
Mafahari wa Real: Bale (kulia) akiwa na wachezaji wenzake wa Madrid (kutoka) Asier Illarramendi, Alvaro Arbeloa, Alvaro Morata, Marcelo Vieira na Xabi Alonso
0 comments:
Post a Comment