Na Prince Akbar, Dar es Salaam
KIUNGO mpya wa Yanga SC, Hassan Dilunga amesema kwamba anaifahamu changamoto iliyopo mbele yake baada ya kusaini timu hiyo, na kwa sababu hiyo anajiandaa kikamilifu kwenda kukabiliana nayo.
“Yanga ina viungo wengi wazuri, ni kweli na ninafurahi kujiunga na timu kama hiyo kwa sababu ni changamoto nzuri kwangu. Nitajibidiisha tu kwa mazoezi ili niwe vizuri niweze kupata nafasi,”alisema.
Dilunga pia aliikana na kuisuta blogu moja iliyoandika eti yeye alikana kusaini Yanga. “Nilisikia, lakini mimi sikuongea nao, nilishangaa sana walizipata wapi zile habari, mimi nimesaini Yanga ni mchezaji wa Yanga,”alisema.
Siku moja baada ya Dilunga kutangazwa amesaini Yanga, blogu moja ‘inayosifika kwa upotoshaji’ iliandika eti mchezaji huyo amekana kusaini Yanga.
Blogu hiyo iliyowahi kutoa kali ya milenia kwa kuandika eti Francis Cheka ndiyo bondia wa kwanza Mtanzania kumpiga Mmarekani, wakati Rodgers Mtagwa na Mambeya Bakari walikwishawapiga mabondia wa nchi hiyo tena nyumbani kwao, imekuwa ikipotosha mambo mengi kutokana uelewa duni wa wahusika wake.

Dilunga akiwatoka wachezaji wa Zimbabwe Jumanne iliyopita akiichezea timu ya taifa, Taifa Stars katika mchezo ulioisha kwa sare ya 0-0 |
“Yanga ina viungo wengi wazuri, ni kweli na ninafurahi kujiunga na timu kama hiyo kwa sababu ni changamoto nzuri kwangu. Nitajibidiisha tu kwa mazoezi ili niwe vizuri niweze kupata nafasi,”alisema.
Dilunga pia aliikana na kuisuta blogu moja iliyoandika eti yeye alikana kusaini Yanga. “Nilisikia, lakini mimi sikuongea nao, nilishangaa sana walizipata wapi zile habari, mimi nimesaini Yanga ni mchezaji wa Yanga,”alisema.
Siku moja baada ya Dilunga kutangazwa amesaini Yanga, blogu moja ‘inayosifika kwa upotoshaji’ iliandika eti mchezaji huyo amekana kusaini Yanga.
Blogu hiyo iliyowahi kutoa kali ya milenia kwa kuandika eti Francis Cheka ndiyo bondia wa kwanza Mtanzania kumpiga Mmarekani, wakati Rodgers Mtagwa na Mambeya Bakari walikwishawapiga mabondia wa nchi hiyo tena nyumbani kwao, imekuwa ikipotosha mambo mengi kutokana uelewa duni wa wahusika wake.
0 comments:
Post a Comment