Na Princess Asia, Dar es Salaam
KIPA wa pili wa Yanga SC, Deo Munishi ‘Dida’ ameweka rekodi ya kusimama langoni kwa dakika 270 bila kuruhusu bao hata moja, timu hiyo ikivuna mabao 10 na pointi tisa, hatimaye kupanda kileleni Ligi Kuu mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara leo.
Dida alianza kudaka mechi na Rhino Rangers wiki iliyopita, Yanga ikishinda 3-0 baada ya kipa wa kwanza, Ally Mustafa ‘Barthez’ kuruhusu mabao matatu ndani ya dakika 45 za kipindi cha pili na timu hiyo kulazimishwa sare ya 3-3 ikitoka kuongoza 3-0 dhidi ya mahasimu Simba SC, Oktoba 20, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Akadaka tena mechi iliyofuata Jumanne, Yanga ikishinda tena 3-0 dhidi ya JKT Mgambo na leo tena amehitimisha dakika 270 bila kufungwa, timu yake ikishinda 4-0 dhidi ya JKT Ruvu.
Hapana shaka, kutokana na kazi nzuri ndani ya mechi tatu katika kipindi hiki ambacho upepo si mzuri kwa Barthez, Dida anaweza kusimama langoni tena katika mchezo wa mwisho wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, dhidi ya JKT Oljoro Novemba 7, mwaka huu.
Barthez alidaka mechi zote tisa za mwanzo za Ligi Kuu za Yanga na kufungwa mabao 11, yakiwemo matatu katika sare ya 3-3 na Simba SC.
Dida alisajiliwa Yanga SC msimu huu, akitokea Azam FC kwa ajili ya kuwa kipa wa pili wa timu hiyo, baada ya kutemwa kwa Mghana, Yaw Berko.
Dida na Barthez wamewahi kudaka pamoja Simba SC kama wasaidizi wa Juma Kaseja, kabla ya kila mmoja kuondoka kwa wakati wake akikimbia benchi.

Dakika 270 bila kufungwa; Deo Munishi 'Dida' nyota yake inang'ara sasa Jangwani |

0 comments:
Post a Comment