MSHAMBULIAJI Mario Balotelli amewachangasha tena mashabiki wake leo baada ya kutweet 'this is the end' (huu ni mwisho) saa kadhaa baada ya kukosa penalti AC Milan ikilazimishwa sare ya 1-1 na Genoa.
Mshambuliaji huyo hatari, alitweet ujumbe huo Kiingerezamajira ya saa 11 Alfajiri kwa sa za kwao katika akaunti yake ya @finallymario.
Pamoja na hayo, saa sita baadaye akatuma ujumbe mwingine wa tweet Kitaliano, uliosomeka: ‘Forza Milan comunque e sempre.’ ambao Kiingereza ni 'Go on Milan, no matter how and forever'.
Mwisho wa barabara? Mario Balotelli alikosa penalti timu yake AC Milan inayosuasua ikilazimishwa sare ya 1-1 na Genoa
Anamaanisha nini? Balotelli ametweet baada ya sare ya AC Milan na Genoa
Balotelli akipiga penalti aliyokosa
Hakuna furaha: Balotelli amekosa penalti mbili msimu huu
0 comments:
Post a Comment