MSHAMBULIAJI Mario Balotelli na wachezaji wenzake wa AC Milan wamewasili Glasgow jana tayari kwa mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya wenyeji Celtic ya Scotland.
Shabiki mmoja wa Scotland akiwa amevalia kwa staili ya Nintendo, Luigi alimfua Balotelli na kupiga naye picha Uwanja wa Ndege.
Mshambuliaji huyo wa Milan anatumaini timu yake itashinda Celtic Park ili kujiwekea mazingira mazuri ya kusonga hatua ya mtoano, wakitoka kufana vibaya katika ligi ya kwao, Serie A.
Super Mario: Nyota wa AC Milan, Mario Balotelli (kulia) akiwa na shabiki aliyevaa kama Luigi mjini Glasgow
Mapokezi mazuri: Balotelli (kulia) alikuwa mwenye furaha kupiga picha na shabiki aliyevalia kama Luigi (kushoto)
0 comments:
Post a Comment