REAL Madrid imeibuka na ushindi wa mabao 5-0 usiku huu dhidi ya Almeria katika Ligi Kuu ya Hispania, maarufu kama La Liga kwenye Uwanja wa Estadio de los Juegos, Mediterráneos.
Cristiano Ronaldo alifunga bao la kwanza dakika ya tatu kwa Real Madrid pasi ya Isco kabla ya kutolewa nje kwa maumivu ya nyama, ambayo kwa sasa yanamuweka nje mpinzani wake mkuu katika tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia, Lionel Messi wa Barcelona pia ya Hispania.
Sasa Mreno huyo yuko shakani kuichezea Real katika mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Galatasaray Jumatano, ingawa baada ya mechi kocha wa Madrid , Carlo Ancelotti alisema: "Cristiano ana matatizo ya nyama, lakini ni mshituko tu, hakuna maumivu makubwa,".
Karim Benzema aliifungia Real bao la pili dakika ya 61 pasi ya Jese Rodriguez kabla ya Gareth Bale kufunga la tatu dakika ya 71, , Isco la nne dakika ya 75 pasi ya Jese Rodriguez na Alvaro Morata kuhitimisha karamu hiyo ya mabao dakika ya 81, pasi ya Casemiro.
Mfalme wa Hispania: Cristiano Ronaldo na Gareth Bale wakishangilia baada ya Real Madrid kupata bao la kwanza
Still going: Real are trying to keep pace with Barcelona at the top of La Liga
Worry: Ronaldo had to leave the pitch due to a hamstring scare, but Carlo Ancelotti tried to allay fears
Simple finish: Bale scored the third for Madrid and his fifth in Real colours
Pace and power: Real Madrid's Cristiano Ronaldo skips past Almeria's Jesus Joaquin Fernandez
In the goals: Xabi Alonso congratulates Ronaldo after the Portugal man scored
Wizard: Bale takes a tumble as Real go on search for another goal
Tricky player: Real midfielder Isco gets past Almeria's Verza
Another: Karim Benzema scored Real's second in there easy win
0 comments:
Post a Comment