KIUNGO Yaya Toure amekumbana na kejeli za kibaguzi akifananishwa na nyani usiku huu Manchester City ikiibuka na ushindi wa 2-1 ugenini dhidi ya CSKA Moscow katika Jiji Kuu la Urusi.
Kelele za kibaguzi zilisikika kutoka mashabiki wa wenyeji katika mchezo ambao City ilinufaika na mabao mawili ya Sergio Aguero ikitoka nyuma na kushinda mechi hiyo ya Li ya Mabingwa Ulaya.
Na City imethibitisha itapeleka malalamiko rasmi UEFA juu ya 'unyama' aliofanyiwa Toure.
"Hakika inaumiza mtu unapozungumza na watu wanaendelea kufanya hivyo,"alilalamika Toure. "Huwezi kuamini na inaniumiza sana upande wangu,".
Inauma: Toure akiwastaajabu mashabiki wabaguzi
Toure ameitaka UEFA kuchukua hatua kali
Mlengwa: Yaya Toure alikumbana na kejeli za kibaguzi kutoka mashabiki mjini Moscow
Heshima: Toure alivaa beji ya kupiga ubaguzi
"Nafikiri UEFA wanahitaji kufanya kitu cha nguvu. Itakuwa vizuri ikiwa watazuia hiyo.
"Baadhi ya nyimbo zilizokuwa zinaimbwa zilikuwa za kipumabvu kabisa, nafikiri UEFA wanatakiwa kufanya kazi. Kila wakati tunasema kitu fulani na inaendelea, kitu fulani lazima kifanyika kuzuia hii,".
Alipoulizwa ni hatua gani ichukuliwe na bodi hiyo ya soka Ulaya, Toure alitaka adhabu zitolewe badala ya faini ndogo ndogo ambazo zimekuwa zikitolewa siku za nyuma.
"Wanahitaji kufanya zaidi,"alisema. "Nafikiri UEFA wanatakiwa kuwa na nguvu, na kuzishika klabu zote na mashabiki wote wanaofanya hivyo (wahusika). Labda kufungia viwanja,".
"Kwangu kama mchezaji wa Afrikan wakati wote imezungumzwa kusikia kwamba mambo kama hayo tunahitaji kufanya kitu juu ya hilo,".
0 comments:
Post a Comment