// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); YANGA SC WAMTUMA KATABARO POINTI TATU BUKOBA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE YANGA SC WAMTUMA KATABARO POINTI TATU BUKOBA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, October 10, 2013

    YANGA SC WAMTUMA KATABARO POINTI TATU BUKOBA

    Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
    MJUMBE wa Kamati ya Utendaji ya Yanga SC, Mussa Katabaro ameteuliwa kuwa mkuu wa msafara wakikosi cha timu hiyo kilichoondoka leo kwa ndege kwenda Bukoba kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Kagera Sugar.
    Sababu moja kubwa ya Yanga SC kumpa jukumu hilo Katabaro ni kwamba, Bukoba ndio nyumbani kwao hivyo uongozi unaamini anaweza kusaidia timu kushinda mechi hiyo ngumu.
    Mkuu wa msafara; Mussa Katabaro anatakiwa kurejea na pointi tatu kutoka Bukoba

    “Mimi Bukoba ni nyumbani na hii si mara ya kwanza kuwa mkuu wa msafara kwa mechi za Bukoba. Najua mchezo utakuwa mgumu kwa sababu Kagera ni timu nzuri, lakini nitajitahidi kutumia uenyeji wangu kule kuisaidia timu kurejea Dar es Salaam na pointi tatu,”alisema Katabaro.  
    Yanga SC imeondoka kwa ndege saa 12:00 asubuhi ya leo kwenda Bukoba, ikipitia Mwanza. Mabingwa hao wa Ligi Kuu wataondoka na kikosi cha wachezaji 21 kwa ajili ya mechi hiyo itakayopigwa Uwanja wa Kaitaba.  
    Kikosi hicho ni makipa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Deo Munishi ‘Dida’ na Yussuf Abdul, mabeki wa pembeni; Juma Abdul, Mbuyu Twite, Oscar Joshua na David Luhende na mabeki wa kati Kevin Yondan na Nadir Haroub ‘Canavaro’. 
    Wengine ni viungo Athumani Iddi ‘Chuji’, Frank Domayo, Haruna Niyomzima na Nizar Khalfan, wakati mawinga ni Simon Msuva, Mrisho Ngassa na Abdallah Mnguli ‘Messi’ na washambulaji ni Didier Kavumbangu, Hamisi Kiiza, Said Bahanuzi, Jerry Tegete na Hussein Javu.  
    Yanga SC inashika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ikiwa na pointi 12, ikizidiwa na tatu na Simba SC walio kileleni na mbili na Azam FC walio nafasi ya pili. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC WAMTUMA KATABARO POINTI TATU BUKOBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top