Na Mahmoud Zubeiry, Bukoba
MSHAMBULIAJI wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Fumo Felician alikuwa mmoja wa walioshuhudia mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya timu yake ya zamani, Yanga SC ya Dar es Salaam dhidi ya wenyeji Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba, Bukoba juzi. Baada ya mchezo huo, ambao Yanga SC ilishinda mabao 2-1, BIN ZUBEIRY ilifanya mahojiano na mshambuliaji huyo wa zamani wa Pamba SC ya Mwanza aliyekuwa na umbo kubwa. Endelea.
BIN ZUBEIRY: Habari za siku nyingi kaka
FUMO: Salama tu
BIN ZUBEIRY: Vipi siku hizi unaisha huku?
FUMO: Hapana, mimi bado nipo Mwanza, nilikuja kuangalia mechi tu
BIN ZUBEIRY: Niambie, uliionaje mechi kwa ujumla
FUMO: Ilikuwa nzuri, kila timu ilicheza kwa uwezo wake, Yanga walicheza mfumo wa ugenini, walijua watakabiliwa na ushindani mkubwa, hawakutaka kuchezea mipira kwenye eneo lao. Kagera walikuwa wameahidiwa vitu vingi wakishinda mechi na walicheza vizuri kwa kujituma, ila bahati haikuwa yao. Yanga walinifurahisha kupata bao la mapema, baada ya hapo wakalilinda hadi mapumziko, kipindi cha pili Kagera wakasawazisha, wakaja juu kusaka bao la ushindi. Kagera ilitawala vizuri sehemu ya kiungo. Yanga walipoteana dakika kama 15 za kwanza kipindi cha pili. Kilichowasaiadia Yanga ni uzoefu. Kagera kitimu ni wazuri. Isipokuwa nadhani mchecheto wa mechi uliwaponza kwa sababu, walicheza na timu kubwa, kama wangetulia wangepata mabao zaidi ya mawili kabla ya mapumziko.
BIN ZUBEIRY: Hali ya ushindani katika mechi hiyo umeionaje ukilinganisha na wakati wenu mnacheza
FUMO: Ushindan ni tofauti sana, wakati ule nipo Yanga tulipokuwa tunakuja Kagera, morali ya mechi ilikuwa ni kubwa kuanzia kwa wachezaji hadi wapenzi. Wakati ule Kagera ilikuwa timu nzuri, ina wachezaji wazuri kuliko sasa, mechi ilikuwa na ushindani mkubwa, tulikuwa tunawafunga kwa tabu sana. Wakati mwingine sare au na wao wanatufunga.
BIN ZUBEIRY: Ubora wa timu katika mechi hiyo na wakati wenu mnacheza, na hata kwa wachezaji mmoja mmoja ukoje?
FUMO: Mtu aliyeingia uwanjani, akisoma majina ya kikosi cha Yanga, yalikuwa yanatisha, lakini hawakucheza kitimu. Kagera walicheza kitimu, Yanga walitumia uzoefu tu. Kagera walicheza vizuri, walikuwa wana uwezo wa kupiga pasi analau hadi sita au nane, ndiyo maana nimekuambia Yanga jana walicheza mpira wa ugenini. Yanga bahati nzuri ilikuwa na watu kama Mbuyu Twite, Kevin Yondan na Nadir Canavaro pale nyuma wanajua kuosha (kuokolea mbali), mpira ulikuwa hauchezwi katikati.
BIN ZUBEIRY: Uwezo wa wachezaji mmoja mmoja…
FUMO: Wakati wetu kwa mchezaji mmoja mmoja, mfano kipa Steven Nemes, alikuwa ana uwezo mkubwa si sawa na Barthez (Ally Mustafa), ukichukulia mchezaji mmoja mmoja, bado sisi tulikuwa tuna uwezo mkubwa kuliko sasa hivi. Tatizo kubwa la sasa hivi, timu nyingi zina viungo wa kawaida, si wachezaji wa uwezo mkubwa sana, tofauti na zamani, mfano Yanga na Pamba zilipokuwa zinakutana mimi bado nipo Pamba, Yanga wanakuwa na watu kama Athumani China na Issa Athumani (marehemu) pale katikati. Pamba tulikuwa tuna Mao Mkami, Nico Bambaga (marehemu) au Hussein Marsha kabla hajahamia Simba SC. Walikuwa wana uwezo mkubwa sana na wabinifu, mpira lazima uwe na viungo wa vile.
BIN ZUBEIRY: Uwezo wa Mrisho Ngassa hivi sasa ukilinganisha na enzi za Edibily Lunyamila, nani zaidi?
FUMO: Lunyamila bado alikuwa juu, kasi ya Lunyamila huwezi kufananisha na ya Ngassa. Ngassa anaonekana ana kasi kubwa, ni mzuri zaidi kwa sababu sasa hivi hakuna mabeki wazuri, ndiyo maana anaonekana mzuri. Ni sawa sawa na Juma Kaseja amedaka muda mrefu na bado anaonekana bora, kwa sababu hakukutana na washambliaji wa nguvu. Hajapata mikiki ya washambuliaji kama wakati wetu.
BIN ZUBEIRY: Uwezo wa wachezaji wengine kwa ujumla sasa na wakati wenu?
FUMO: Mechi ya Yanga na Kagera kwa mfano, dakika 90 zote hakuna shuti la maana lililopigwa langoni, inakuwa ngumu hata kumjua kipa mzuri.
BIN ZUBEIRY: Asilimia 80 ya wachezaji wa Kagera si wa hapa Bukoba, unadhani kwa nini?
FUMO: Vijana wengi wazaliwa wa Bukoba, wanatoka hapa wanakwenda mikoa mingine si kwa mambo ya mpira, bali kwa ajili ya masomo, wazazi wengi wamewekeza kwenye elimu, wanaona kama mpira hauna mpango wowote. Ndiyo maana Kagera wachezaji wengi wanatoka nje. Tofauti za zamani wachezaji wengi walikuwa wa hapa hapa akina Hussein Kaitaba, Project Muta, Nkama Ntare na wengine.
BIN ZUBEIRY: Lakini mpira ni mchezo wa watoto wa mtaani zaidi na tunaona wachezaji wapo na wanacheza na timu zipo Bukoba…
FUMO: Labda sasa hapo tatizo lipo kwenye uongozi wa mkoa.
BIN ZUBEIRY: Kwa nini Kagera kuna timu moja tu Ligi Kuu na ni mkoa mkubwa?
FUMO: Hilo ni tatizo ambalo lipo Mwanza pia. Kagera wana timu kongwe inaitwa Balimi, ni timu ambayo ingepanda ingekuwa ina mashabiki wengi kwa sababu wanaamini ndiyo timu ya wazawa. Kagera Sugar wanaamini ni timu ya kuja tu. Na pia bado Usimba na Uyanga upo sana Bukoba. Kagera inapocheza na Ashanti watu hawaendi uwanjani. Lakini ikija Yanga au Simba, watu wanakwenda kuzipokea na kuzisaidia zishinde.
BIN ZUBEIRY: Wewe mwenyeji wa Bukoba, ile umekulia Mwanza na umecheza Pamba, niambie Mwanza, hakuna timu Ligi Kuu kwa sasa, tatizo nini na ni mkoa mkubwa ule?
FUMO: Ilifikia wakati watu walifurahia hata hiyo Toto African iliposhuka daraja. Walikuwa wanaudhika kitu kimoja, Toto inapocheza ligi inakamia mechi ya Simba tu. Ikicheza na Simba wanavyocheza, hadi unasema wangecheza hivi siku zote ni mabingwa, hata ilipoteremka watu wakasema bora iteremke tu.
BIN ZUBEIRY: Lakini Mwanza mji mkubwa, kwa nini Toto tu?
FUMO: Tatizo pia ni Usimba na Uyanga, watu wamaamini Toto tawi la Yanga, Pamba tawi la Simba, fitina bado zipo pale pale, wanamalizana wenyewe. Hakuna mikakati ya kimkoa.
BIN ZUBEIRY: Tunajua tatizo la Pamba ni tangu itemwe na Bodi ya Pamba, angalia Mbeya, baada ya kuona hawawezi kuipata Tukuyu Stars nyingine, sasa wana Mbeya City, timu ya Halmashauri ya Jiji. Kwa nini Mwanza wasiwe na timu ya aina hiyo, Halmashauri ya Jiji la Mwanza ina mapato makubwa.
FUMO: Hadi Toto kufika pale, Mkuu wa Mkoa (Everist Ndukilo) alijitahidi sana, tatizo bado Usimba na Uyanga, hakupata sapoti. Na itachukua muda Mwanza kupata timu nyingine Ligi Kuu. Viongozi wa sasa wa chama cha mkoa wanaingia kwa maslahi yao. Wanakuja kutangaza majina baadaye wagombee ubunge, hawana dhamira ya kusaidia soka.
BIN ZUBEIRY: Vipi Halmashauri ya Jiji kuwa na timu kama Mbeya?
FUMO: Wazo zuri na kwa sababu sasa hivi Mwanza tuna Meya ambaye ni mtu wa michezo, mheshimiwa Mabula na bado kijana na mtu ambaye mimi ni rafiki yangu, nitakaa naye nimpe mikakati hiyo.
BIN ZUBEIRY: Wadogo zako pia walicheza soka Francis (Kagera) na Fortunatus (Toto), kwa sasa wako wapi?
FUMO: Wapo Mwanza wana shughuhli zao, nao wamestaafu.
BIN ZUBEIRY: Na wewe kwa sasa baada ya kustaafu unafanya nini?
FUMO: Nafanya biashara
BIN ZUBEIRY: Ulihusishwa na mauaji ya aliyekuwa RPC wa Mwanza, Kamanda Ballo, ilikuwaje na imekuaje uko huru sasa?
FUMO: Walinihisi kwa sababu yule dada aliyekuwa na marehemu RPC Ballo kabla ya kuuawa, alikuwa mpenzi wa kaka yangu (Felix), sasa wakahisi labda tumehusika, lakini baada ya uchunguzi ikagundulika sisi hatukuhusika. Walioua walishikwa nasi tukaachiwa huru.
BIN ZUBEIRY: Habari za kifamilia?
FUMO: Nina mke (Angela) na watoto wawili (Flavia miaka 12 na Fratern miaka saba)
BIN ZUBEIRY: Naona uko juu juu, basi nichukue muda wako sana, nashukuru kwa leo.
FUMO: Haina shaka, nashukuru pia.
BIN ZUBEIRY: Sawa, safari njema, wasalimie Mwanza.
FUMO: Asante, nawe ukisafiri, safiri salama, wasalimie Dar es Salaam, tutaonana Oktoba 20 (siku Simba na Yanga zitamenyana).

Yanga haichezi kitimu; Fumo Felician mshambuliaji wa zamani wa Yanga SC amesema timu hiyo inatisha kwa majina, lakini si soka |

Kikosi cha Yanga SC 1994, Fumo Felician wa nne kutoka kulia na kushoto |
BIN ZUBEIRY: Uwezo wa wachezaji mmoja mmoja…
FUMO: Wakati wetu kwa mchezaji mmoja mmoja, mfano kipa Steven Nemes, alikuwa ana uwezo mkubwa si sawa na Barthez (Ally Mustafa), ukichukulia mchezaji mmoja mmoja, bado sisi tulikuwa tuna uwezo mkubwa kuliko sasa hivi. Tatizo kubwa la sasa hivi, timu nyingi zina viungo wa kawaida, si wachezaji wa uwezo mkubwa sana, tofauti na zamani, mfano Yanga na Pamba zilipokuwa zinakutana mimi bado nipo Pamba, Yanga wanakuwa na watu kama Athumani China na Issa Athumani (marehemu) pale katikati. Pamba tulikuwa tuna Mao Mkami, Nico Bambaga (marehemu) au Hussein Marsha kabla hajahamia Simba SC. Walikuwa wana uwezo mkubwa sana na wabinifu, mpira lazima uwe na viungo wa vile.
BIN ZUBEIRY: Uwezo wa Mrisho Ngassa hivi sasa ukilinganisha na enzi za Edibily Lunyamila, nani zaidi?
FUMO: Lunyamila bado alikuwa juu, kasi ya Lunyamila huwezi kufananisha na ya Ngassa. Ngassa anaonekana ana kasi kubwa, ni mzuri zaidi kwa sababu sasa hivi hakuna mabeki wazuri, ndiyo maana anaonekana mzuri. Ni sawa sawa na Juma Kaseja amedaka muda mrefu na bado anaonekana bora, kwa sababu hakukutana na washambliaji wa nguvu. Hajapata mikiki ya washambuliaji kama wakati wetu.
Fumo akiwa na BIN ZUBEIRY Bukoba |
BIN ZUBEIRY: Uwezo wa wachezaji wengine kwa ujumla sasa na wakati wenu?
FUMO: Mechi ya Yanga na Kagera kwa mfano, dakika 90 zote hakuna shuti la maana lililopigwa langoni, inakuwa ngumu hata kumjua kipa mzuri.
BIN ZUBEIRY: Asilimia 80 ya wachezaji wa Kagera si wa hapa Bukoba, unadhani kwa nini?
FUMO: Vijana wengi wazaliwa wa Bukoba, wanatoka hapa wanakwenda mikoa mingine si kwa mambo ya mpira, bali kwa ajili ya masomo, wazazi wengi wamewekeza kwenye elimu, wanaona kama mpira hauna mpango wowote. Ndiyo maana Kagera wachezaji wengi wanatoka nje. Tofauti za zamani wachezaji wengi walikuwa wa hapa hapa akina Hussein Kaitaba, Project Muta, Nkama Ntare na wengine.
BIN ZUBEIRY: Lakini mpira ni mchezo wa watoto wa mtaani zaidi na tunaona wachezaji wapo na wanacheza na timu zipo Bukoba…
FUMO: Labda sasa hapo tatizo lipo kwenye uongozi wa mkoa.
Fumo na rafiki zake Bukoba |
BIN ZUBEIRY: Kwa nini Kagera kuna timu moja tu Ligi Kuu na ni mkoa mkubwa?
FUMO: Hilo ni tatizo ambalo lipo Mwanza pia. Kagera wana timu kongwe inaitwa Balimi, ni timu ambayo ingepanda ingekuwa ina mashabiki wengi kwa sababu wanaamini ndiyo timu ya wazawa. Kagera Sugar wanaamini ni timu ya kuja tu. Na pia bado Usimba na Uyanga upo sana Bukoba. Kagera inapocheza na Ashanti watu hawaendi uwanjani. Lakini ikija Yanga au Simba, watu wanakwenda kuzipokea na kuzisaidia zishinde.
BIN ZUBEIRY: Wewe mwenyeji wa Bukoba, ile umekulia Mwanza na umecheza Pamba, niambie Mwanza, hakuna timu Ligi Kuu kwa sasa, tatizo nini na ni mkoa mkubwa ule?
FUMO: Ilifikia wakati watu walifurahia hata hiyo Toto African iliposhuka daraja. Walikuwa wanaudhika kitu kimoja, Toto inapocheza ligi inakamia mechi ya Simba tu. Ikicheza na Simba wanavyocheza, hadi unasema wangecheza hivi siku zote ni mabingwa, hata ilipoteremka watu wakasema bora iteremke tu.
BIN ZUBEIRY: Lakini Mwanza mji mkubwa, kwa nini Toto tu?
FUMO: Tatizo pia ni Usimba na Uyanga, watu wamaamini Toto tawi la Yanga, Pamba tawi la Simba, fitina bado zipo pale pale, wanamalizana wenyewe. Hakuna mikakati ya kimkoa.
BIN ZUBEIRY: Tunajua tatizo la Pamba ni tangu itemwe na Bodi ya Pamba, angalia Mbeya, baada ya kuona hawawezi kuipata Tukuyu Stars nyingine, sasa wana Mbeya City, timu ya Halmashauri ya Jiji. Kwa nini Mwanza wasiwe na timu ya aina hiyo, Halmashauri ya Jiji la Mwanza ina mapato makubwa.
FUMO: Hadi Toto kufika pale, Mkuu wa Mkoa (Everist Ndukilo) alijitahidi sana, tatizo bado Usimba na Uyanga, hakupata sapoti. Na itachukua muda Mwanza kupata timu nyingine Ligi Kuu. Viongozi wa sasa wa chama cha mkoa wanaingia kwa maslahi yao. Wanakuja kutangaza majina baadaye wagombee ubunge, hawana dhamira ya kusaidia soka.
BIN ZUBEIRY: Vipi Halmashauri ya Jiji kuwa na timu kama Mbeya?
FUMO: Wazo zuri na kwa sababu sasa hivi Mwanza tuna Meya ambaye ni mtu wa michezo, mheshimiwa Mabula na bado kijana na mtu ambaye mimi ni rafiki yangu, nitakaa naye nimpe mikakati hiyo.
BIN ZUBEIRY: Wadogo zako pia walicheza soka Francis (Kagera) na Fortunatus (Toto), kwa sasa wako wapi?
FUMO: Wapo Mwanza wana shughuhli zao, nao wamestaafu.
BIN ZUBEIRY: Na wewe kwa sasa baada ya kustaafu unafanya nini?
FUMO: Nafanya biashara
BIN ZUBEIRY: Ulihusishwa na mauaji ya aliyekuwa RPC wa Mwanza, Kamanda Ballo, ilikuwaje na imekuaje uko huru sasa?
FUMO: Walinihisi kwa sababu yule dada aliyekuwa na marehemu RPC Ballo kabla ya kuuawa, alikuwa mpenzi wa kaka yangu (Felix), sasa wakahisi labda tumehusika, lakini baada ya uchunguzi ikagundulika sisi hatukuhusika. Walioua walishikwa nasi tukaachiwa huru.
Pozi; Fumo Felician wa sasa |
BIN ZUBEIRY: Habari za kifamilia?
FUMO: Nina mke (Angela) na watoto wawili (Flavia miaka 12 na Fratern miaka saba)
BIN ZUBEIRY: Naona uko juu juu, basi nichukue muda wako sana, nashukuru kwa leo.
FUMO: Haina shaka, nashukuru pia.
BIN ZUBEIRY: Sawa, safari njema, wasalimie Mwanza.
FUMO: Asante, nawe ukisafiri, safiri salama, wasalimie Dar es Salaam, tutaonana Oktoba 20 (siku Simba na Yanga zitamenyana).
0 comments:
Post a Comment