USIJALI sana Arsene – bila shaka itakuwa bahati ya mara ya 10 wakati Jose Mourinho na timu yake, Chelsea watakapokwenda Uwanja wa Emirates
Jumatatu ya Desemba 23, mwaka huu.
Kipigo cha Arsenal cha mabao 2-0 katika Kombe la Ligi maarufu kama Capital One kutoka kwa Chelsea usiku wa jana ilikuwa ni mara ya tisa Wenger anakutana na Mourinho na kutoka kichwa chini.
Rekodi yake dhidi ya Mreno huyo inamaanisha yeye ni mnyonge: amefungwa mara tano na kutoa sare nne. Anapotokea Mourinho, Wenger ni kibonde sana.
Katika mechi hiyo ya Kombe la Ligi, ambayo Arsenal
ilibadilisha wachezaji nane wa kikosi cha kwanza na Chelsea 10 na bado Wenger alichapwa.
Kipigo cha Arsenal cha mabao 2-0 katika Kombe la Ligi maarufu kama Capital One kutoka kwa Chelsea usiku wa jana ilikuwa ni mara ya tisa Wenger anakutana na Mourinho na kutoka kichwa chini.
Rekodi yake dhidi ya Mreno huyo inamaanisha yeye ni mnyonge: amefungwa mara tano na kutoa sare nne. Anapotokea Mourinho, Wenger ni kibonde sana.
Ubabe pale pale: Ushindi wa Chelsea kwa Arsenal unamfanya Jose Mourinho aendeleze rekodi ya kutofungwa na Arsenal Wenger (chini)
Mourinho na Wenger walisalimiana kabla ya mechi ya Kombe la Ligi jana
Spacial Juan: Juan Mata akishangilia kumuwezesha kocha Chelsea kuendeleza ubabe wake kwa Wenger
Mara nyingine tena: Didier Drogba akipiga kichwa pembeni ya Phillippe Senderos katika Fainali ya Kombe la Ligi mwakia 2007 katika mechi nyingine Mourinho anamfunga Wenger
MOURINHO v WENGER
Des 12 2004 | Arsenal 2 Chelsea 2 | Ligi Kuu |
Apr 20 2005 | Chelsea 0 Arsenal 0 | Ligi Kuu |
Ago 7 2005 | Chelsea 2 Arsenal 1 | Ngao ya Jamii |
Ago 21 2005 | Chelsea 1 Arsenal 0 | Ligi Kuu |
Des 18 2005 | Arsenal 0 Chelsea 2 | Ligi Kuu |
Des 12 2006 | Chelsea 1 Arsenal 1 | Ligi Kuu |
Feb 25 2007 | Chelsea 2 Arsenal 1 | Fainali Kombe la Ligi |
Mei 6 2007 | Arsenal 1 Chelsea 1 | Ligi Kuu |
Okt 29 2013 | Arsenal 0 Chelsea 2 | Kombe la Ligi |
Ametulia chini: Lakini Mourinho naye ni kibonde wa Pep Guardiola
0 comments:
Post a Comment