KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger bado hajaiondoa katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya England, Manchester United.
The Gunners wamepaa kileleni mwa Ligi Kuu kufuatia ushindi wa 4-1 dhidi ya Norwich na sasa wanaizidi kwa pointi nane timu ya David Moyes, baada ya Mashetani hao Wekundu kukubali bao la kusazishiwa la dakika za mwishoni la Southampton Jumamosi.
Wenger, pamoja na hayo hataki kuwaondoa mabingwa hao watetezi katika mbio za ubingwa, wakati Arsenal ikijiandaa kwa safari ya Old Trafford mwezi ujao baada ya kumenyana na vigogo wengine England, Liverpool.
"Ni mapema mno. Hawako nje ya mbio za ubingwa," amesema Wenger. "Tunazizi pointi mbili tu timu nyingine zote. Man United wapo nje ya mbio za taji? Hapana, lakini ukweli pengo a pointi 10 mwanzoni ni dogo,".
Wenger ameendelea: "Kama ni kuchagua, unataka kuwa kileleni katika mbio, lakini huwezi kuiondoa Man United leo.
"Wana wachezaji wakubwa, uzoefu mkubwa na wao ni klabu kubwa. (kuwa na pointi zaidi) ni wastani wa mechi tatu, ambayo ni haraka sana katika ligi yetu,".
Wamefulia: United walipoteza pointi tena mwishoni mwa wiki safari hii ugenini mbele ya Southampton
0 comments:
Post a Comment