MSHAMBULIAJI Robinho alionyesha utundu wa hali ya juu wa kuuchezea mpira jana katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya timu yake AC Milan dhidi ya Barcelona.
Katika dakika ya tatu alifanya vitu adimu akimtoka Alexis Sanchez kwa kumvisha kanzu moja matata sana.
Bahati mbaya kwa mshambuliaji huyo wa Milan, alipoteza mpira huo baada ya Mbrazil mwenzake, Dani Alves kutokea na kuondosha mpira kwenye hatari.
Tutaonana baadaye: Robinho akiinua mpa kwa ustadi wa hali ya juu kumtoka Alexis Sanchez kwa kumbisha kanzu
Mbrazil mwenzake Robinho, Neymar, pia alikuwepo uwanjani usiku wa jana, amekwishawaonyesha mashabiki mavituz kadhaa siku za nyuma yenye kudhihirisha uwezo wake mkubwa wa kuchezea mpira. Lakini wawili hao ni baadhi tu ya wanasoka waliowahio ,kuonyesha utundu wao wa hali ya juu katika soka, BIN ZUBEIRY inakukumbusha wakali wengine leo.
Kanzu: Robinho hata hivyo alipoteza mpira kwa Dani Alves
Robinho aliuinua mpira kwa miguu yake yote miwili, hakika ni ufundi wa hali ya juu
Neymar
Neymar alionyesha moja ya sababu nyingi za Barcelona kutoa Pauni Milioni 50 kumsajili. Hiyo ilikuwa katika mechi baina ya timu yake ya zamani, Santos dhidi ya Bolivar ya Bolivia. Mabeki lazima wachukie kucheza dhidi ya kijana huyu.
Paul Gascoigne
Moja kati ya vipaji adimu kuwahi kutokea England katika miaka 30 iliyopita alifunga moja ya mabao bora kabisa katika Euro 96 Uwanja wa Wembley.
Dennis Bergkamp
Hata Bergkamp alifanya mambo ya ajabu katika ushindi wa Arsenal wa 2-0 dhidi ya Newcastle kwenye Ligi Kuu a England Machi mwaka 2002, baada ya Mholanzi huyo.
Gianfranco Zola
Hakuna ajabu Chelsea walikuwa wanajiandaa kumbakiza Zola baada ya kutishia kuondoka mwaka 2003 na katika mechi ya Kombe la FA mwaka 2002 dhidi ya Norwich Uwanja wa Stamford Bridge alionyesha yeye ni nani.
Jay-Jay Okocha
Bolton chini ya kocha Sam Allardyce ilikuwa ina mtaalamu mmoja kutoka Afrika anaitwa Jay-Jay Okocha ambaye aliwafanya kitu mbaya Arsenal mapema mwaka 2003.
Matty Burrows
Roy alifunga bonge la bao katika dakika za majeruhi, Rovers ikimenyana na Portadown ambalo liliingia katika kinyang'anyiro cha tuzo ya bao bora la mwaka 2010.
Joseph Ndo
Akiwa amekwenda na Cameroon katika Fainali za Kombla Dunia mwaka 1998 na 2002, Ndo alifanya vyema sana katika miaka yake tisa ya kucheza Ireland. Lakini pasi ya kisigino kwenda kwa mchezaji mwenzake waakati akiichezea Sligo Rovers mwaka jana ilionyesha mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 36 anastahili kuit timu ya taifa.
Rodrigo Palacio
Bora zaidi ya Zola? Inawezekana. Palacio wa Genoa kuna mavituz yamebaki Serie A baada ya kukukimbia kutoka langoni kukutana na kona dhidi ya Lazio msimu uliopita dhidi ya Spurs katika mechi ya Europa League timu hizo zikitoka sare ya 0-0.
Cristiano Ronaldo
Uthibitisho kwamba El Clasico siyo tu wachezaji 22 wanaojaribu kushinda mpira wa adhabu. Hi inatokana na mavituz aliyoyafanya Ronaldo akiifungia Real Madrid bao la kuongoza dhidi ya Barcelona, Agosti.
Neymar
Kudhihirisha kwamba Neymar ana uwezo mkubwa – hapa ni kati ya mambo ya ajabu aliyowahi kuyafanya katika maisha yake Santos katika mechi dhidi ya Atletico Mineiro Oktoba.
Jon Otsemobor
Osvaldo Ardiles
0 comments:
Post a Comment