MECHI ATAKAZOKOSA TORRES
CHELSEA
Okt 6 v Norwich (A)
Okt 19 v Cardiff (H)
Okt 22 v Schalke (A)
Okt 27 v Man City (H)
HISPANUA
Okt 11 v Belarus (H)
Okt 15 v Georgia (H)
MSHAMBULIAJI Fernando Torres anatumai kurejea uwanjani baada ya wiki tatu, kufuatia kuumia goti juzi nchini Romania.
Torres alitolewa nje dakika za mwanzoni katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa, Chelsea ikishinda 4-0 dhidi ya Steaua Bucharest Jumanne, lakini vipimo vimethibitisha hana maumiu makubwa.
Arakosa safari ya Norwich Jumapili, ambayo tayari asingecheza kwa sababu ya kutumikia adhabu kutokana na di nyekundu aliyopewa dhidi ya Tottenham.
Anatarajiwa kurudi kuichezea Hispania katika mechi za kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Belarus na Georgia, lakini Chelsea wanatumai kuwa naye tena mshambuliaji wao huyo kabla ya mwishoni mwa mwezi.
Maumivu: Fernando Torres akitibiwa na madaktari wa Chelsea baada ya kuumia goti dhidi ya Steaua Bucharest
Mdogo mdogo: Torres akitoka nje dakika ya 11 juzi kumpisha Samuel Eto'o baada ya kuumia