// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); TIMU MPYA TISHIO JIJINI YAANZISHWA NI SAPPHIRE FC YA ABDULFATAH - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE TIMU MPYA TISHIO JIJINI YAANZISHWA NI SAPPHIRE FC YA ABDULFATAH - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, October 15, 2013

    TIMU MPYA TISHIO JIJINI YAANZISHWA NI SAPPHIRE FC YA ABDULFATAH

    Na Princess Asia, Dar es Salaam
    UONGOZI wa Sapphire Court Hotel ya Kariakoo, Dar es Salaam umeanzisha timu ambayo itakuwa ikishikriki mashindano mbalimbali nchini, imeelezwa.
    Mkurugenzi wa Sapphire, Abdulfatah Salim Saleh amesema kwamba timu hiyo itakayokuwa ikiundwa na wafanyakazi wake, itakuwa na maskani yake Vijibweni, Kigamboni, Dar es Salaam.
    Sapphire FC, tishio jipya Jijini

    “Michezo ni furaha, michezo ni upendo, michezo inaunganisha watu, lakini pia michezo ni afya, kwa kuzingatia haya nikaona bora tuanzishe hii timu ambayo itakuwa tishio hapa Dar es Salaam,”alisema Saleh.
    Mpwa huyo wa kocha na mchezaji wa zamani wa Simba SC, Hassan Afif amesema kwamba atahakikisha anaihudumia vizuri timu hiyo ili iwe na hadhi inayoendana na Sapphire na kwa kuanzia ameitengea bajeti ya Sh. Milioni 100.
    “Tayari nimeweka benki Sh. Milioni 100 kwa ajili ya hii timu, itahudumiwa kila kitu, sisi tunathamini wafanyakazi wetu, tunataka na wao wafurahi,”alisema rafiki huyo kipenzi wa Nahodha wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars , kipa Juma Kaseja.  

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TIMU MPYA TISHIO JIJINI YAANZISHWA NI SAPPHIRE FC YA ABDULFATAH Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top