Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA OKTOBA 2, 2013 SAA 12:40 JIONI
MSANII maarufu wa vichekesho, Kitale ambaye amejizolea umaarufu kwa kuigiza kama teja, yuko katika matayarisho ya filamu mpya ya vichekesho iliyobeba hadithi ya kusisimua.
Kitale ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, filamu hiyo itakwenda kwa jina la Chizi Kalogwa Tena na atacheza pamoja na wasanii wenzake kadhaa, wakiwemo Jengua na Ringo.
Amesema filamu hiyo imefanywa na kampuni The Mak Productions ya Dar es Salaam na imehusisha maeneo kadhaa Jijini, yakiwemo Kijichi na Mji Mwema Ungindoni. Kigamboni.
Amesema filamu hiyo inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi huu na kuingia sokoni mapema mwezi ujao na amewataka wapenzi wa muvi nchini kujiandaa kupata kitu kikali.
Kitale alijipatia umaarufu wake katika kundi la Vituko Show la Tanga alipoibuka pamoja na marehemu Sharo Milionea.
Hata hivyo, katika kujitafutia maslahi zaidi akaamua kuachana na kundi hilo na kuanza kufanya kazi zake mwenyewe na tangu amejitoa Vituko Show hii itakuwa filamu yake ya tano.
Baadhi ya filamu zake nyingine zilizofanya vizuri ni Impossible na Nawaektia, wakati pia anafanya muziki na wimbo wake maarufu ni Hili Dude na yuko mbioni kutoa wimbo mpya utakaokwenda kwa jina Nawaektia, alioutengeneza katika studio za Mazuu Records.

Chizi Kalogwa Tena; Kitale alipokuwa kwenye upigaji picha wa filamu yake mpya leo Mji Mwema Ungindoni |