“Mmekuwa kumbukumbu bora kwenye maisha yangu. Nimefanikiwa kuongoza baadhi ya wachezaji bora nchini. Yale mabao ya dakika za majeruhi, kufanikiwa kushinda tukitokea nyuma, hata kufungwa yote ni sehemu ya klabu yetu bora. Kazi yenu sasa ni kusimama nyuma ya kocha wetu mpya.”
Hivi ndivyo linavyosomeka bango kubwa lililopo kwenye jukwaa la Sir Alex Ferguson stand pale Old Trafford, maneno hayo ya kutia hamasa ni maneno ya kwa heri ya kocha wao wa zamani.
Inawezekana kabisa yalichaguliwa ilikuwa moyo wa subira mashabiki kwa utawala mpya wa David Moyes, baada ya miaka 27 timu ikiwa chini ya Ferguson hakuna aliyejua mashabiki watayachukulia mabadiliko.
Hakuna aliyedhani kwamba mchakato wa kubadilisha kocha utakuwa rahisi.
Maneno: Tangazo kama hili liliwekwa Old Trafford, likuwa na maneno ya mwisho ya hotuba ya kwa heri ya Sir Alex Ferguson
Na kweli haujawa rahisi, Sare ya 1-1 dhidi ya Southampton wiki iliyopita ilizidi kumkatisha tamaa. Kikosi cha Mauricio Pochettino kinafanya vizuri na ni ngumu kuwafunga, lakini kwa timu inayotaka ubingwa zile ndiyo mechi za kushinda.
Vichapo kutoka kwa Liverpool na Manchester City vinaweza kutetewa. Kwa Liverpool kisasi tayari kimelipwa kwenye Kombe la Capital One mwezi uliopita.
Kufungwa nyumbani na West Bromwich Albion kuliibua mashaka. Ule utamaduni wa kufunga mabao muhimu kwenye dakika za majeruhi unaonekana kuanza kupotea.
United wameshacheza mechi kadhaa msimu huu kwenye michuano yote. Na wamekuwa kwenye kiwango chao cha kawaida kwenye mechi mbili tu.
Viatu vikubwa: Kuvaa viatu vya Sir Alex Ferguson siyo kazi ndogo
Kwenye ushindi wa 4-1 dhidi ya Swansea na ushindi wa 4-2 dhidi ya Bayer Leverkusen kikosi cha Moyes kilionyesha soka safi la kushambulia, lakini timu zote hizi mbili zlionekana kupoteana.
Ni mapema mno kusema majanga yananukiwa Old Trafford, lakini kwa kila pointi inayopotea ndivyo ubingwa unavyozidi kupotea. Arsenal wanazidi kushika kazi mbele ya United kwa sasa.
Japokuwa unaweza kuona mashimo kwenye kikosi kidogo cha Arsene Wenger ikifika wakati wa Krismass ndipo majanga yataanza kugeukia Emirates – kikosi cha kwanza cha Arsenal ni kizuri sana.
Je Moyes alaumiwe kwa kushuka huku? Bado hana kikosi cha kwanza. - David De Gea, Patrice Evra, Michael Carrick, Rooney na Van Persie ndiyo wanauhakika wa namba, wengine wote leo wanacheza kesho wanasugua benchi.
Ameanza msimu na beki ya Evra-Ferdinand-Vidic-Jones, lakini kikosi kilichocheza na Southampton kilikuwa na Evra-Evans-Jones-Rafael. Hii inaonyesha jinsi gani ambavyo timu haijatulia.
Amewatumia Ashley Young, Nani na Antonio Valencia kwa nyakati tofauti. Shinji Kagawa amekuwa akiwekwa benchi mara kwa mara na hata akianza hamalizi dakika 90.
Cha kusifiwa Moyes ni kumtambulisha rasmi Adnan Januzaj na dogo huyo hajamuangusha katika mechi ya Sunderland, alifunga mabao mawili maridadi na hata kwenye mechi ya Southampton yeye ndiye alikuwa mmoja kati ya wachezaji bora wa Man United.
Marouane Fellaini ameshindwa kuthibitisha ubora wake tangu alipsajili. Anaonekana kutokujua majukumu yake kwenye timu.
Hajitambui: Marouane Fellaini ameshinda kwenda na kasi ya Manchester United
Hiyo yote inaweza kubadilika mwaka mmoja kutoka sasa na mawigi yake Fellaini yakaanza kuvaliwa upya kwenye jukwaa la Sir Alex Ferguson.
Kumlaumu Moyes kwa Man United kushindwa kufanya usajili wakati wa kiangazi itakuwa sawa na kumuonea. Alimtaka Mbelgiji hiyo na amempata.
Pale Arsenal wanapotumia fedha nyingi zaidi yako kwenye soko la usajili inabidi ujiulize.
Wenger amevunja rekodi yake ya usajili kwa kumsajili Mesut Ozil, Chelsea wamenasa wachezaji kadhaa, akiwemo Samuel Eto'o na Andre Schurrle, Manchester City wamesajili kila waliyemtaka (kasoro Isco), wakati Tottenham wametumia vizuri fedha yao ya Gareth Bale
Moyes alihitaji wachezaji wenye majina makubwa kuboresha kikosi chake, lakini alishindwa kuwapata. Timu inamatatizo.
Ferguson aliamua kutokuziba shimo la kiungo, kwa kumtumia Ryan Giggs na kumrudisha Paul Scholes aliyekuwa amestaafu. Japokuwa usajili wa Fellaini ulikuwa wa kukurupuka, lakini mtu anaweza kusema kwamba alijaribu kutatua tatizo.
Anahitaji Makamu Mwenyekiti, Ed Woodward kujipanga upya ili wasichemke tena kwenye usajili.
Saini: Ed Woodward (kushoto) akishuhudia Adnan Januzaj (katikati) akijifunga mkataba wa miaka mitano
Biashara bora kwa timu zinazotaka ubingwa ilikuwa kubakiza mastaa wake, United kumzia Rooney kuondoka na Liverpool kukomaa na Luis Suarez awape ubingwa wa kwanza tangu mwaka 1990.
Ferguson anaamini kwamba iwapo Moyes atapata taji msimu huu anastahili pongezi nyingi. Lakini Moyes anaonekana kuongea kama vile hana uhakika iwapo atapata ubingwa msimu wowote.
Baki: Kumbakiza Wayne Rooney ilikuwa biashara bora kwa United wakati wa kiangazi.
Kumponda kwa kuwa mkimya na kukubali kila kitu ni kosa, lakini mashabiki wa United hawajazoea kuwa na kocha anayekubali kushindwa kirahisi.
Moyes anaweza kuwa mbuzi wa kafara, lakini kikosi kilichocheza na Southampton kilitosha kuwaua.
Hakuna tiba ya kipindi cha mpito, lakini muda, kutokuwa na haraka na sapoti vitasaidia. United wanatakiwa kuimarisha kikosi chao Januari.
0 comments:
Post a Comment