// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMBA SC WAINGIZA MILIONI 60 PAMBANO NA PRISONS JANA TAIFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMBA SC WAINGIZA MILIONI 60 PAMBANO NA PRISONS JANA TAIFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, October 13, 2013

    SIMBA SC WAINGIZA MILIONI 60 PAMBANO NA PRISONS JANA TAIFA

    Na Boniface Wambura, Dar es Salaam 
    Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya wenyeji Simba na Tanzania Prisons kutoka Mbeya iliyochezwa jana (Oktoba 12 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 60,521,000.
    Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mechi hiyo namba 55 na kushuhudiwa na watazamaji 10,494 waliokata tiketi kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.
    Kikosi cha Simba SC jana

    Kila klabu ilipata mgawo wa sh. 14,191,002.55 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 9,232,016.95.
    Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 7,215,763.96, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 4,329,458.37, Kamati ya Ligi sh. 4,329,458.37, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,164,729.19 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,683,678.26.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC WAINGIZA MILIONI 60 PAMBANO NA PRISONS JANA TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top