WAKATI Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ikiingia katika mzunguko wake wa nane, Simba SC imefanikiwa kukaa kileleni kwa kukusanya pointi 15 ndani ya mechi saba, kutokana na kushinda mechi nne na kutoa sare tatu, ikiwazidi pointi tatu mabingwa watetezi, Yanga SC.
Simba SC ilifulia msimu uliopita baada ya kupokonywa ubingwa na wapinzani wa jadi, Yanga SC waliofuatiwa na Azam FC.
Kwa misimu miwili mfululizo sasa Azam sasa imeweza kuiengua moja ya klabu hizo kongwe katika michuano ya Afrika na bila shaka mwaka huu kwa maandalizi yao mazuri, wataweka tofauti kidogo katika msimu mpya.
Misimu miwili iliyopita, Azam imekuwa ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu, kwanza nyuma ya Simba SC na baadaye nyuma ya Yanga SC na dhamira kuu ya wamiliki wa klabu hiyo msimu huu ni ubingwa.
Mara kadhaa nimewahi kuandika juu ya umuhimu wa ustawi wa klabu hizo mbili, Simba na Yanga SC kwa sababu ndizo zinanazoteka hisia za wengi miongoni mwetu katika kupambana na viongozi mafedhuli na mafisadi ambao wanaingia kuongoza klabu hizo kwa manufaa yao.
Na hilo haliwezi kubadilika mara moja, uimara wowote wa Azam hautabadilisha kitu kwa Simba na Yanga ni sawa tu na Manchester United na Liverpool pale England, pamoja na kwamba Wekundu wa Anfield wamefulia kwa muda sasa, bado wao kwa pamoja na Mashetani Wekundu ndiyo klabu kubwa nchini humo.
Na uimara wa upinzani wa jadi, unatokana na uimara wa timu zote- kuwa katika hali nzuri kiushindani ili kuweza kuwavutia mashabiki wake. Tumeona msimu uliopita Simba SC wakipitia katika wakati mgumu, migogoro ikitawala katika kila nyanja.
Wachezaji walifukuzwa, makocha walibadilishwa na uongozi ulitiwa misukosuko- hakika haikuwa hali nzuri na si vyema ikajirudia. Kitu kimoja kikubwa katika Simba na Yanga ambacho wapenzi wanajali, matokeo mazuri.
Hawahitaji kuwa na maendeleo kama klabu nyingine mfano tu Azam FC achilia mbali TP Mazembe, bali ubingwa wa Bara na kumfunga mtani, haijalishi hata wakitolewa Raundi ya kwanza michuano ya Afrika. Mradi mpinzani kaadabishwa na taji wamechukua.
Na kwa sababu hii, ndiyo maana Azam inawapita kama wamesimama Simba na Yanga, kwa sababu dira na malengo ni tofauti. Azam wanaumia kuona Mazembe imecheza Klabu Bingwa ya Dunia wao bado- lakini Simba na Yanga zinaoneana wivu zenyewe na ndiyo maana kila siku zinagombea wachezaji zenyewe kwa zenyewe, hazina hata ndoto za kuwa japo na Uwanja wa mazoezi. Huruma!
Tumeiozea hali hiyo na tumekwishaandika sana sana juu ya hayo, lakini viongozi wake wameziba nta masikioni na zaidi tunaambulia kuchukiwa tu, kisa kuwaambia watu ukweli- ama kweli duniani lazima wawepo wajinga ili uwajue weledi.
Kuna hali fulani inaanza kujitokeza Simba SC dhidi ya benchi ya benchi la Ufundi la klabu hiyo- baada ya mechi dhidi ya Ruvu Shooting iliyoisha kwa sare ya 1-1 Alhaj Abdallah Kibadeni na Msaidizi wake, Jamhuri Kihwelo wanaanza kuonekana hawafai.
Watu wanasema Simba SC ilicheza chini ya kiwango siku hiyo kwa makocha hawafai- jamani fikra hizi si za kisoka. Dunia nzima, wakati timu bora inacheza ovyo na kufungwa, hayo mambo yanatokea kwenye soka.
Lakini hilo tu la kutazama, bila shaka wakati Jose Mourinho anarejea Chelsea na ni kipindi hicho hicho Kibadeni anarejea Simba SC- unaweza kuona hata The Blues bado haijatulia na kocha huyo Mreno amekuwa akikiri juu ya ugumu unaomkabili katika kuweka mambo sawa.
Hata Kibadeni amekuwa akisema- anahataji muda, ni kweli anastahili kupewa muda.
Ningependa sana kuwaasa wana Simba leo kwa ujumla- baada ya kupitia msimu mgumu, hatimaye wametulia na kuanza kuandaa timu yao upya. Viongozi wametekeleza majukumu yao vizuri kwa kuanzia kusajili, kuajiri kocha mpya, kuiweka timu kambini mapema na kuipatia mechi nyingi za kujipima nguvu.
Kocha mzawa na gwiji wa zamani wa klabu hiyo, Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden’ amechukua nafasi ya Mfaransa, Patrick Liewig na baada ya kuisuka timu kwa takriban miezi mitatu, ameingia kwenye ligi na matunda yake timu ipo kileleni.
Simba SC wamemchukua Kibadeni baada ya kuvutiwa na kazi yake akiwa Kagera Sugar ambako mwishoni mwa msimu alipewa tuzo ya kocha bora wa Ligi Kuu- hakuna shaka huyu ni bora na wazi hata bila kuangalia rekodi ya msimu uliopita, Chifu Mputa ni bora.
Ndiye huyu ambaye aliifikisha Simba SC fainali ya Kombe la CAF mwaka 1993 na wengi wanaamini alihujumiwa ndiyo maana hakuchukua taji. Usajili ambao Simba SC imepeleka TFF juzi ni uliofanywa na Kibadeni. Aliwahakiki wachezaji, akaridhia uwezo wao akabariki wasajiliwe.
Simba SC ni kama wanaanza kujipanga upya baada ya kupitia katika msimu mgumu na wa vurugu nyingi- na mababu zetu walisema kitambo kirefu, mwanzo mgumu. Simba SC lazima kwanza watambue wapo katika hatua ya mwanzo ya kujiimarisha upya, ambayo ni ngumu.
Hata David Moyes alifanya kazi nzuri Everton iliyoishawishi bodi ya Ukurugenzi ya Manchester United kumrithisha mikoba ya Sir Alex Ferguson, lakini tunaona amekuwa katika mwanzo mbaya Old Trafford.
Simba SC waweke fikra zao kwamba, wanajenga timu upya na wawape muda makocha na wachezaji ili wajipange, hatimaye kufikia uwezo wa kushindana na Yanga na Azam, ambao kwa hakika wako vizuri kwa sasa zaidi yao.
Mashabiki wawe nyuma ya timu yao kwa sasa kwa matokeo yoyote ili kuwapa moyo makocha na wachezaji wafanye kazi yao vizuri. Kuna kukosea sana tu katika hatua za mwanzoni, ila baada ya kujifunza kiasi cha kutosha, hadithi itabadilika. Dhahiri.
Ni ngumu kufanya kazi Simba na Yanga kwa ufanisi kwa sababu ya presha ya mashabiki na hata Kibaden analijua hilo, lakini alikubali tu kujilipua kuacha kazi klabu ambayo isingemfukuza leo wala kesho na kwenda klabu ambayo anaweza kufukuzwa hata saa moja baada ya kusaini Mkataba.
Ipo haja ya kuheshimu uwezo wa mtu, historia hata na rekodi. Kwa haya yote Kibadeni ni bora na amekwishadhihirisha hapo hapo Msimbazi si chini ya mara tatu. Anajua anachokifanya. Kikubwa tu ni kupewa sapoti na kila anayejiita Simba SC, ili hata kama si msimu ujao, basi utakaofuata atimize ndoto zake.
Simba SC hawajui tu, lakini King Kibaden ndiye mtu ambaye anafaa kuwa kocha wao hadi atakaposema yeye mwenyewe basi. Kwanza ni Simba damu, pili ni mwalimu wa mpira kitaaluma, tatu amecheza soka na anaijua vyema, nne mzoefu kwa ujumla na tano, ni mtu mzima mwenye hekima na busara. Wiki njema.

0 comments:
Post a Comment