SHABIKI SIMBA AKIMBIZWA TEMEKE HOSPITALI TAABAN, ABDULFATAH WA SAPPHIRE NAYE AKIONA CHA MOTO
Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam MWANACHAMA wa Simba wa tawi la Mpira Pesa, Magombeni, Dar es Salaam, Fii Kambi amekimbizwa hospitali ya Temeke kwa matibabu zaidi baada ya kujeruhiwa katika vurugu zilizotokea Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya SImba na Kagera Sugar ya Bukoba. Uwanja wa Taifa leo uligeuka eneo la vita baina ya Polisi mashabiki wa Simba SC, kufuatia Kagera Sugar kupata bao la kusawazisha dakika ya pili ya muda wa nyongeza baada ya kutimia kwa dakika 90 za mchezo timu hizo zikitoka 1-1.
Shabiki wa SImba, Fii Kambi akiwa amelazwa katika Zahanati ndogo ya Uwanja wa Taifa
Baada ya Salum Kanoni kukwamisha nyavuni mkwaju wake wa penalti, mashabiki wa Simba waliokuwa viti vya Rangi ya Bluu na Chungwa, walianza kung’oa viti na kuvitupia uwanjani. Mara moja, Polisi walianza kupambana na mashabiki hao kwa kuwatupia mabomu ya machozi, ndipo wakaanza kukimbia. Makocha na wachezaji wa Simba kwa pamoja waliwafuata waamuzi kuwalalamikia- hali ambayo ilifanya watolewe kwa kusindikizwa na Polisi. Simba ilitangulia kufunga kupitia kwa Amisi Tambwe dakika ya 45.
Fii anapelekwa kwenye gari akimbizwe hospitali ya Temeke
Amelazwa
Anapelekwa hospitali Temeke
Abdulfatah ameporwa simu ya Sh. Mlioni 1.8
Kutokana na vurugu hizo mashabiki wengi walijeruhiwa na kupatiwa huduma katika Zahanati ndogo ya Uwanja wa Taifa na wengine waliondoka na maumivu yao. Watu pia waliporwa simu, fedha na vitu mbalimbali vya thamani. Miongoni mwa walioporwa ni mmiliki wa hoteli ya Sapphire Court, Abdulfatah Salim Saleh wakati anateremka jukwaani, akaibiwa simu yake aina ya Blackberry Q10, yenye thamani ya Sh. Milioni 1.8. “Tunateremka kukawa na tatizo na milango ya kutokea watu wengi mlango mdogo, milango mingine imefungwa, sasa pale watu wengi tu wameibiwa wengine walikuwa wanalia kuibiwa pochi za fedha zina dola,”alisema Abdulfatah.
Lookman crowned African footballer of the year
-
The 2024 Confederation of African Football (CAF) Award took center stage on
Monday night, with the best talents in African football emerging winners.
The...
Edozie Njoku and the new APGA
-
By Ambrose Ododo it has been a long and tortuous journey for the birth of
the rebranded All Progressives Grand Alliance, APGA, and it looks like it
is go...
Reports: Jack Wilshere set for Arsenal return
-
Former Arsenal midfielder Jack Wilshere has held talks with the north
London side on one of its vacant academy coaching roles. Under 23 manager
Per Mertes...
YANGA ‘KUPAA’ JUMANNE KUIFUATA MWADUI FC
-
MARA baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Namungo Fc kwenye uwanja wa
Majaliwa, Lindi, siku ya jumapili, Kikosi cha Young Africans Sports Club,
kitareje...
0 comments:
Post a Comment