Mmiliki wa Hotel ya Kimataifa Sapphire Hotel Bw Abdulfatah Salim akimpa vifaa vya michezo Kaptain msaidizi wa MK Rangers FC Bw. Emanuel Kidagayo
Mmiliki wa Hotel ya Kimataifa Sapphire Hotel Bw Abdulfatah Salim akimpa vifaa vya michezo Kaptain msaidizi wa MK Rangers FC Bw. Emanuel Kidagayo
Na Mwandishi Wetu, Kariakoo
KATIKA kuhakikisha inaendelea kukuza na kuthamini michezo hapa nchini na kusaidia jamii, Hivi karibuni Hotel ya Kimataifa iliyopo jijini Dar es salaam iliweza kuwasaidia vijana wa MK Rangers FC wa Kitunda Mwanagati vifaa vya michezo vikiwemo jezi pamoja na mipira.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY, mmiliki wa hoteli hiyo ya kimataifa, Abdulfatah Salim Saleh alisema; "Maendeleo ya Mtanzania hayawezi kuja na kukua bila ya sisi Watanzania wenyewe kusaidiana na kushiriki kwenye mchakato mzima wa kuleta maendeleo na sisi Sapphire Hotel tumeona haja ya kuwasaidia hawa vijana kukuza vipaji vyao vya mpira kwa kuwapatia vifaa hivi na haswa haswa itawasaidia kuwaondoa vijiweni na kuanza mambo ya kihuni na badala yake watakuwa salama kwenye michezo'
Aliendelea kusema, ‘Ni vyema kwa taasisi mbalimbali, makampuni pamoja na mahoteli mengine makubwa kutoa misaada kuanzia chini haswa haswa kwa vijana wadogo wadogo kama hawa badala ya kuendelea misimamo yao ya kutoa misaada kwenye timu kubwa kubwa tu maana mpira wa Tanzania utaanzia chini kwenda juu na wasipo wasaidia watoto kama hawa basi soka la Tanzania lipo kwenye hati hati kufa.’
Ikumbukwe hii sio mara ya kwanza kwa Hotel hii ya kimataifa kutoa misaada hapa Tanzania na kuendelea kusaidia vijana kwenye nyanja mbali mbali haswa haswa ikiwemo ajira kwenye hotel hii ya kimataifa.
Sapphire Hotel hipo maeneo ya Kariakoo mtaa wa Sikukuu/ Lindi Street.
Website: www.sapphirecourthotel.com
0 comments:
Post a Comment