// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SAMATTA NA ULIMWENGU WAIPA MAZEMBE TAJI LA SUPER CUP DRC KWA USHINDI WA 7-0 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SAMATTA NA ULIMWENGU WAIPA MAZEMBE TAJI LA SUPER CUP DRC KWA USHINDI WA 7-0 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, October 13, 2013

    SAMATTA NA ULIMWENGU WAIPA MAZEMBE TAJI LA SUPER CUP DRC KWA USHINDI WA 7-0

    Na Prince Akbar, Lubumbashi, DRC
    TOUT Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) leo imetwaa taji la Super Cup la nchini humo baada ya kuifumua mabao 7-0 FC MK ya Kinshasa mjini Lubumbashi.
    Mabingwa hao mara nne Afrika tayario walikuwa mbele kwa mabao mawili hadi mapumziko, yaliyofungwa na mshambuliaji Mtanzania, Thomas Ulimwengu dakika ya 21 na kiungo wa Ghana, Daniel Nii Adjei dakika ya 33.
    Mbwana Samatta akiwa ameinua taji la Super leo Lubumbashi

    Dakika tano baada ya kuanza kipindi cha pili, Gladson Awako wa Ghana pia alifunga la tatu kabla ya ndugu yake Richard Kissi Boateng kufunga la nne dakika ya 66.
    Adjei akafunga bao lake la pili katika mchezo huo dakika ya 68 kabla ya Herve Ndonga kufunga la sita dakika tatu baadaye na Mtanzania mwingine, Mbwana Samatta akafunga la saba dakika ya mwisho.
    Ushindi huo mnono unakuja siku chache kabla ya kucheza Nusu Fainali ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Stade Malien ya Mali wiki ijayo, baada ya awali kushinda ugenini 2-1 katika mchezo wa kwanza.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAMATTA NA ULIMWENGU WAIPA MAZEMBE TAJI LA SUPER CUP DRC KWA USHINDI WA 7-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top