MASHABIKI wa Arsenal wamejawa hofu baada ya kuona picha za kiungo Jack Wilshere akiwa ameinua mguu wake akipozwa maumivu kwa barafu baada ya kutolewa nje na kukaa benchi.
Wilshere alianza kwenye kikosi cha The Gunners kilichomenyana na Borussia Dortmund katika Ligi ya Mabingwa Ulaya dakika ya 58 wakati huo timu hizo zikiwa zimefunana bao 1-1.
Santi Cazorla akaingia kuchukua nafasi ya Wilshere Uwanja wa Emirates na mwishowe Arsenal ikalala 2-1 mbele ya wababe hao wa Ujerumani.
Kiungo huyo England mwenye umri wa miaka 21, alijigonga nyuma ya lango la Roman Weidenfeller katika harakati za kugombea mpira kipindi cha kwanza.
Alimalizia daika chache za kipindi cha kwanza kabla ya kocha Arsene Wenger kumtoa mapema kipindi cha pili.
Ameumia: Wilshere akiwa ameshika kifundo cha mguu wake wa kulia nyuma la lango katika mchezo huo
Maumivu: Wilshere alionekana hayuko vizuri baada ya kulala chini
Wilshere alipigwa picha akiwa amekaa sambamba na wachezaji wengine wa akiba amevaa jaketi la Arsenal na mguu wake umefunikwa kwa barafu.
Licha ya mabadiliko hayo, Wilshere anaamini atakuwa fiti kwa mchezo wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Crystal Palace mwishoni mwa wiki.
Kazini: Wilshere akipambana katika safu ya kiungo jana ya Arsenal jana
Katika mchezo huo, Henrikh Mkhitaryan aliwafungia wageni bao la kuongoza kabla ya mshambuliaji pekee wa Arsenal, Olivier Giroud kukisawazisha kikosi cha Wenger.
Lakini Robert Lewandowski, mfungaji bora wa Dortmund, akawamaliza Arsenal nyumbani kwa bao la dakika za lala salama.
0 comments:
Post a Comment