WINGA Wilfried Zaha amechezea mechi mbili kikosi cha wakubwa cha timu ya taifa ya England msimu huu, zote Uwanja wa Wembley, siku nne tofauti, mwezi Agosti.
Wiki nane baadaye winga huyo aliyenunuliwa na Manchester United kwa Pauni Milioni 15 ameshuka kwa kiasi kikubwa.
Wiki nane baadaye winga huyo aliyenunuliwa na Manchester United kwa Pauni Milioni 15 ameshuka kwa kiasi kikubwa.
Tangu aichezee mechi ya Ngao ya Jamii klabu hiyo, na za kirafiki dhidi ya Scotland kwa timu yake ya taifa, Zaha amefulia ile mbaya.
Hasomeni tena Man United – na sasa amezidiwa kete na kinda wa miaka 18, Adnan Januzaj.
Anapigwa baridi: Wilfried Zaha (kushoto) aliachwa benchi kikosi cha England U-21 kikimenyana na San Marino
Hasomeki tena: Zaha amecheza mechi tu Manchester United msimu huu - ya Ngao ya Jamii
Mambo yamezidi kuwa magumu kwake katika soka ya kimataifa, baada ya kukosa nafasi hata ya kuchezea timu ya vijana chini ya umri wa miaka 21, baada ya Zaha kuwekwa benchi Alhamisi usiku timu hiyo ikishinda mabao 4-0 kwenye Uwanja wa Saido Berahino dhidi ya San Marino.
David Moyes, kocha ambaye hashawishiki kumpa nafasi kinda huyo, anazidi kukata tamaa na mchezaji huyo aliyeuwa mfalme Crystal Palace.
Kwa ujumla mam ni magumu kwa Zaha ambaye analipwa mshahara wa Pauni 35,000 kwa wiki kutokana na mkataba wake aliosaini na United Januari. Tatizo nini?
Pozi la mshambuliaji: Zaha alikuwa mkali wa mabao Crystal Palace timu hiyo ikipanda Ligi Kuu msimu uliopita
Bado anapambana: Lakini Zaha, bado anapambana kwa juhudi za mazoezi ili kurejea katika nafasi yake
0 comments:
Post a Comment