Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam JAMAL Emil Malinzi, usiku huu ameshinda Urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kupata kura 72, dhidi ya 52 za mpinzani wake Athumani Jumanne Nyamlani. Katika uchaguzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa NSSF Water Front, Dar es Salaam, Walace Karia alifanikiwa kushinda nafasi ya Makamu wa Rais kwa kupata kura 67 akiwashinda Nassib Ramadhani kura 52 na Imani Madega sita.
Huyu ndiye Rais wenu mpya TFF; Rais aliyemaliza muda wake TFF, Leodegar Tenga kushoto akimtambulisha Jamal Malinzi kuliakuwa Rais mpya wa shirikisho hilo usiku nwa kuamkia leo ukumbi wa NSSF Water Front, Dar es Salaam
Kwa upande wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji walioshinda ni Kalilo Samson (Kanda namba 1- Geita na Kagera) aliyepata kura 102 za ndiyo na 17 za hapana. Kanda namba 2- Mara na Mwanza, mshindi ni Vedastus Lufano aliyepata kura 51 dhidi ya Jumbe Odessa Magati (11), Mugisha Galibona (24), na Samwel Nyalla (39). Epaphra Swai ndiye mshindi wa Kanda namba 3- Shinyanga na Simiyu kwa kura 63 dhidi ya Mbasha Matutu aliyepata 61. Kanda namba 4- Arusha na Manyara mshindi ni Omali Walii Ali aliyepata kura 53 dhidi Elley Mbise (51), Ally Mtumwa (19). Kanda namba 4- Kigoma na Tabora, mshindi ni Ahmed Idd Mgoyi aliyepata kura 92 dhidi ya 28 za Hamisi Yusuf Kitumbo.
Tenga akimkabidhi mpira Malinzi kuashiria yeye ndiye kiongozi mpya mkuu wa soka nchini
Anampa shada la maua ishara ya kumuachia madaraka
Kwaherini; Tenga akiwaaga Wajumbe
Ayubu Nyaulingo na Blassy Mghube Kiondo ameshinda Kanda namba 6- Katavi na Rukwa kwa kura 73 dhidi ya Ayubu Nyaulingo aliyepata 52. Ayoub Shaibu Nyenzi ndiye mshindi wa Kanda namba 7- Iringa na Mbeya kwa kupata kura 59 na kuwapiku David Samson Lugenge (8), John Exavery Kiteve (12) na Lusekelo Elias Mwanjala (46). Kanda namba 8- Njombe na Ruvuma inawakilishwa na James Patrick Mhagama aliyepata kura 93 dhidi ya 31 za Kapteni mstaafu Stanley William Lugenge. Athuman Kingombe Kambi ndiye mshindi wa Kanda namba 9- Lindi na Mtwara kwa kura 84 akiwazidi Francis Kumba Ndulane (30) na Zafarani Mzee Damoder (11).
Anamkabidhi Katiba ya TFF
Anapongezwa na Mwenyekiti wa Azam FC, Sheikh Said Muhammad Said Abeid
Hussein Zuberi Mwamba ametetea ujumbe wa Kanda namba 10- Dodoma na Singida kwa kura 63 akiwapiku Stewart Masima (58) na Charles Komba (4). Geofrey Irick Nyange ameshinda Kanda namba 11- Morogoro na Pwani akipata kura 78 dhidi ya Juma Pinto (26), Farid Nahdi (14), Riziki Juma Majala (5) na Twahil Twaha Njoki (2). Kanda namba 12- Kilimanjaro na Pwani, Khalid Abdallah Mohamed ndiye aliyeibuka kidedea kwa kura 69 dhidi ya 54 za mpinzani wake Davis Elisa Mosha. Kidao Wilfred Mzigama ameshinda Kanda namba 13- Dar es Salaam kwa kupata kura 60 dhidi ya wapinzani wake Muhsin Said Balhabou (50), Omar Isack Abdulkadir (10) na Alex Crispine Kamuzelya (4).
Kamati mpya ya Utendaji TFF
Wadau Musley Ruwey kushoto na Said Tuliy kulia walikuwepo hadi mwisho
Lookman crowned African footballer of the year
-
The 2024 Confederation of African Football (CAF) Award took center stage on
Monday night, with the best talents in African football emerging winners.
The...
Edozie Njoku and the new APGA
-
By Ambrose Ododo it has been a long and tortuous journey for the birth of
the rebranded All Progressives Grand Alliance, APGA, and it looks like it
is go...
Reports: Jack Wilshere set for Arsenal return
-
Former Arsenal midfielder Jack Wilshere has held talks with the north
London side on one of its vacant academy coaching roles. Under 23 manager
Per Mertes...
YANGA ‘KUPAA’ JUMANNE KUIFUATA MWADUI FC
-
MARA baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Namungo Fc kwenye uwanja wa
Majaliwa, Lindi, siku ya jumapili, Kikosi cha Young Africans Sports Club,
kitareje...
0 comments:
Post a Comment