// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); NGASSA HATARINI KUIKOSA MECHI YA SIMBA JUMAPILI, YANGA WAJIFUA KWENYE JUA KALI PEMBA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE NGASSA HATARINI KUIKOSA MECHI YA SIMBA JUMAPILI, YANGA WAJIFUA KWENYE JUA KALI PEMBA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, October 14, 2013

    NGASSA HATARINI KUIKOSA MECHI YA SIMBA JUMAPILI, YANGA WAJIFUA KWENYE JUA KALI PEMBA

    Na Nurat Mahmoud, Pemba
    YANGA SC tayari ipo kambini kisiwani Pemba kujiandaa na mchezo dhidi ya wapinzani wao wa jadi, Simba SC Jumapili mzunguko wa kwanza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, lakini mshambuliaji Mrisho Khalfan Ngassa yuko hatarini kuukosa mchezo huo.
    Ngassa anasumbuliwa na Malaria na ameanza kutumia dawa jana, ingawa leo mchana alijilazimisha kufanya mazoezi na wenzake kidogo kidogo Uwanja wa Gombani kabla ya kurejea kupumzika katik hoteli ya Samail walipofikia.
    Mrisho Ngassa baada ya kuwasili Pemba, lakini kijana anasumbuliwa na Malaria

    Yanga SC iliyoondoka Dar es Salaam kwa ndege ya kukodi leo asubuhi, ililazimika kufanya mazoezi mchana kwa sababu jioni kuna mechi ya Ligi Kuu ya Zanzibar kwenye Uwanja huo wa nyasi bandia.
    Akizungumzia afya yake, Ngassa alisema hadhani kama itamkosesha kucheza mechi ya Jumapili, kwani ana matumaini ya kupona haraka.
    “Dozi namaliza kesho na siku bado zipo, pamoja na hayo nafanya mazoezi mepesi mepesi, naamini hadi siku ya mechi nitakuwa fiti kabisa, kikubwa naomba wanachama na wapenzi wa Yanga waniombee dua nipone ili niisaidie timu Jumapili,”alisema.
    Athumani Iddi 'Chuji' na Didier Kavumbangu nyuma wakiwa ndani ya ndege kuelekea Pemba


    Kelvin Yondan ndani ya ndege

    Ngassa anasubiriwa kwa hamu Jumapili kuichezea Yanga dhidi ya timu yake ya msimu uliopita Simba SC aliyojiunga nayo akitokea Azam.
    Inaaminika Ngassa ana hasira na Simba SC kutokana na mashabiki wa timu hiyo kumzomea kila anapochezea Yanga na anatarajiwa kujibu Jumapili kwa kucheza kwa bidii kuipatia ushindi timu yake.
    Simba SC imeendelea kuweka kambi yake katika hoteli ya Bamba Beach, Kigamboni kwa ajili ya mchezo huo.
    Katika mechi za mwisho, Simba SC ilishinda 1-0 dhidi ya Prisons Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, wakati Yanga ilishinda 2-1 dhidi ya Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba, Bukoba. 
    Mgonjwa Ngassa akipata kifungua kinywa Pemba, kulia Jerry Tegete na aliyesimama ni Meneja Hafidh Saleh
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NGASSA HATARINI KUIKOSA MECHI YA SIMBA JUMAPILI, YANGA WAJIFUA KWENYE JUA KALI PEMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top