Na Mahmoud Zubeiry, Bukoba
MSHAMBULIAJI Konstantin Trauttmann kutoka Ujerumani nchi anayotokea pia kiungo wa Arsenal ya England, Mesut Ozil, ameomba kusajiliwa na Kagera Sugar acheze mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana mjini hapa, Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 19, mshambuliaji mrefu amesema kwamba ameona ataimudu Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na kuisaidia Kagera.
Konstantin ambaye kwa sasa anachezea timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Kagera Sugar, amesema kwamba baada ya kuona mechi kadhaa za Ligi Kuu za Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba, ameona kabisa anaweza kuhimili vishindo vya ligi hiyo.
Konstantin ambaye anafanya kazi na taasisi ya Jambo Bukoba kwa Mkataba wa mwaka mmoja tangu Agosti mwaka huu, amesema kwa kuwa atamaliza Mkataba wake Agosti mwakani, anaweza kuichezea Kagera katika mzunguko wa pili.
“Nimeambiwa kuna dirisha dogo (la usajili) Januari na ligi itakwenda hadi Mei (2014), nafikiri nikipata nafasi naweza kucheza na kuisaidia Kagera Sugar,”alisema na kuongeza;
“Nimeonyesha uwezo wangu hapa nikicheza timu ya U-20 kwa kufunga mabao na kufanya vizuri kwa ujumla, naamini naweza kufanya hivi hata timu ya wakubwa, wakinipa nafasi nitawasaidia,”alisema.
Kontsantine alisema alipokuwa Ujerumani alikuwa anachezea timu ya vijana chini ya umri wa 20 ya Fortuna Koln ya nchini humo hivyo hana shaka akipewa nafasi Kagera Sugar ataisaidia timu hiyo.
MSHAMBULIAJI Konstantin Trauttmann kutoka Ujerumani nchi anayotokea pia kiungo wa Arsenal ya England, Mesut Ozil, ameomba kusajiliwa na Kagera Sugar acheze mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana mjini hapa, Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 19, mshambuliaji mrefu amesema kwamba ameona ataimudu Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na kuisaidia Kagera.
Anaomba kucheza Ligi Kuu Bara; Konstantin Trautmann anaomba kusajiliwa Kagera Sugar acheze mzunguko wa pili wa Ligi Kuu |
Konstantin ambaye kwa sasa anachezea timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Kagera Sugar, amesema kwamba baada ya kuona mechi kadhaa za Ligi Kuu za Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba, ameona kabisa anaweza kuhimili vishindo vya ligi hiyo.
Konstantin ambaye anafanya kazi na taasisi ya Jambo Bukoba kwa Mkataba wa mwaka mmoja tangu Agosti mwaka huu, amesema kwa kuwa atamaliza Mkataba wake Agosti mwakani, anaweza kuichezea Kagera katika mzunguko wa pili.
Mzungu Kaitaba; Konstatin akiichezea U20 ya Kagera jana Uwanja wa Kaitaba |
Anabadilisha nguo baada ya mechi |
“Nimeonyesha uwezo wangu hapa nikicheza timu ya U-20 kwa kufunga mabao na kufanya vizuri kwa ujumla, naamini naweza kufanya hivi hata timu ya wakubwa, wakinipa nafasi nitawasaidia,”alisema.
Kontsantine alisema alipokuwa Ujerumani alikuwa anachezea timu ya vijana chini ya umri wa 20 ya Fortuna Koln ya nchini humo hivyo hana shaka akipewa nafasi Kagera Sugar ataisaidia timu hiyo.
0 comments:
Post a Comment