KOCHA David Moyes na Robin van Persie walisimama kwa mazunguo ya faragha kwa muda mrefu kwenye Uwanja wa Manchester United leo.
Timu hiyo ilikuwa inajiandaa kwa mchezo wake wa Ligi ya Mabingwa Ulaya Kundi A dhidi ya Real Sociedad kesho.
Na wawili hao muhimu klabuni hapo kama walikuwa wanazungumzia mambo ya kiufundi au mengineyo, walionekana kwa muda mrefu wakijadiliana wakati wa mazoezi Carrington.
Tatizo, bosi? David Moyes na Robin van Persie walikuwa kwenye mjadala mpana Uwanja wa Carrington
Alitumwa? Bila shaka Mholanzi huyo anafikisha ujumbe kwa Wilfried Zaha...
Amechanganyikiwa: Moyes akionekana aliyepagawa katika mkutano na Waandishi wa Habari kabla ya mechi
Wakati huo huo, Rio Ferdinand na Nemanja Vidic wote walikosa mazoezi, sambamba na Danny Welbeck na Tom Cleverley.
Kuendelea kukosekana kwa mabeki hao wawili wa kikosi cha kwanza cha David Moyes kutawatia hofu mashabiki wa timu hiyo baada ya United kuruhus bao la kusawazisha la kizembe dakika za lala salama Jumamosi wakitoa sare na Southampton.
Vidic alitolewa nje kwenye mchezo huo kutokana na majeruhi wakati Ferdinand amekosa mech mbili zilizopita kwa majeruhi pia.
Hawatakuwepo: Nemanja Vidic (kushoto) na Rio Ferdinand (kulia) hawakufanya mazoezi leo Carrington
Anaanza Ligi ya Mabingwa: Adnan Januzaj akifanya mazoezi na wenzake kwa ajili ya mchezo dhidi ya Real Sociedad
Yuko tayari kwa Ligi ya Mabingwa: Adnan Januzaj alionekana yuko tayari kucheza dhidi ya Real Sociedad
David Moyes akiwafundisha vijana wake leo
Siyo kama Hispania: Man United wakijifua
Moyes amesema majeruhi ya Ferdinand si ya muda mrefu na atakuwa tayari kwa mchezo wa marudiano na timu hiyo ya Hispania wakati United inatazamiwa kuendeleza rekodi yake ya kutofungwa katika mashindano hayo msimu huu.
Adnan Januzaj alishiriki mazoezi hayo makali baada ya kupandishwa kikosi cha United kinachoshiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya na nyota huyo kinda ameonekana kumudu kazi kiasi cha kusababisha kinda mwenzake, Wilfried Zaha awekwe kando.
Darren Fletcher, ambaye hajacheza tangu Desemba mwaka jana amepona maumivu yake naye pia amefanya mazoezi.
Tayari kwa kazi: Wayne Rooney na wenzake wakifanya mazoezi
Amechemsha: Wilfried Zaha amezidiwa kete na Januzaj
Karibu tena: Darren Fletcher (kulia) amerejea kazini
Sema chiiizzz: Anderson (kulia), pembeni ya Javier Hernandez
0 comments:
Post a Comment