// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MICHUANO YA CHALLENGE KUANZA NOVEMBA 27 PASIPOJULIKANA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MICHUANO YA CHALLENGE KUANZA NOVEMBA 27 PASIPOJULIKANA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, October 01, 2013

    MICHUANO YA CHALLENGE KUANZA NOVEMBA 27 PASIPOJULIKANA

    Boniface Wambura, IMEWEKWA OKTOBA 1, 2013 SAA 9:33 ALASIRI
    MICHUANO ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CRCAFA Challenge inayoandaliwa na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) inafanyika Kenya kuanzia Novemba 27 hadi Desemba 12 mwaka huu.
    Nchi wanachama ambazo zinataka kushiriki zinatakiwa kuthibitisha ushiriki wao kwa Sekretarieti ya CECAFA kabla ya Oktoba 20 mwaka huu. Wanachama wa CECAFA ni Burundi, Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Somalia, Sudan, Sudan Kusini, Tanzania, Uganda na Zanzibar.
    Aggrey Morris wa kwanza kushoto waliosimama atachezea Zanzibar

    Michuano hiyo itatanguliwa na Mkutano Mkuu wa CECAFA utakaofanyika Novemba 26 mwaka huu ambao pamoja na mambo mengine utakuwa na ajenda ya uchaguzi. Uchaguzi huo ni kwa ajili ya kujaza nafasi nne za wajumbe wa Kamati ya Utendaji.
    Wajumbe wanaomaliza muda wao ni Sahilu Gebremarian wa Ethiopia ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CECAFA, Abdigaani Saed Arab (Somalia), Tariq Atta (Sudan) na Raoul Gisanura (Rwanda).
    Majina ya wagombea yanatakiwa kuwa yamewasilishwa katika Sekretarieti ya CECAFA kabla ya Oktoba 20 mwaka huu, na yakiwa yamethibitishwa na vyama vyao vya mpira wa miguu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MICHUANO YA CHALLENGE KUANZA NOVEMBA 27 PASIPOJULIKANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top