// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MARADONA ASEMA BAADA YA MESSI, RONALDO NA NEYMAR ANAYEFUATIA KWA UBORA DUNIANI NI BALOTELLI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MARADONA ASEMA BAADA YA MESSI, RONALDO NA NEYMAR ANAYEFUATIA KWA UBORA DUNIANI NI BALOTELLI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, October 17, 2013

    MARADONA ASEMA BAADA YA MESSI, RONALDO NA NEYMAR ANAYEFUATIA KWA UBORA DUNIANI NI BALOTELLI

    Living legend: Argentina hero Diego Maradona took part in a question and answer session in Milan on Thursday
    Gwiji hai: Shujaa wa Argentina, Diego Maradona alikuwepo kwenye kipindi cha maswali na majibu mjini Milan Jumatano


    GWIJI wa soka duniani, Diego Maradona amesema kwamba Mario Balotelli ni mwanasoka nambari nne kwa ubora hivi sasa duniani baada ya Messi, Ronaldo na Neymar.
    Katika kipindi cha maswali na majibu mjini Milan, gwiji huyo wa Argentina alielezea mapenzi yake kwa nyota huo wa zamani wa Manchester City na kwamba walianza kufahamiana vyema na mshambuliaji huyo wa Italia alipomtumia picha anavuta cigar ya Cuba. 
    Namba 10 huyo wa zamani, mmoja wa wanasoka bora kabisa kuwahi kutokea duniani alisema: "Mawasiliano yangu ya kwanza na Mario ni pale aliponitumia picha yake anavuta Cuban. Naipenda! Nilicheza,".

    Shabiki mkubwa: Maradona ameelezea namna alivyoshibana na Mario Balotelli (chini) baada ya Mtaliano huyo kumtumia picha
    Mario Balotelli
    Maradona pia anataka kukutana na Balotelli ili ampe ushauri nasaha mshambuliaji huyo wa AC Milan.
    "[Watu lazima] wamuache na amani. Ningependa kuzungumza na Mario peke yetu, katika chumba chetu, na kumfafanulia uzoefu mbaya wote niliopitia.'
    Mario Balotelli
    Characters: Maradona is keen to speak with Balotelli and tell him of the bad experiences he's had in the game
    Watu wa vituko: Maradona anapenda kuzungumza na Balotelli na kumpa uzoefu wa maisha mabovu aliyopitia katika mchezo huo
    Number one: Maradona claimed compatriot Lionel Messi was the world's best player with Balotelli fourth
    Namba moja: Maradona amesema Muargentina mwenzake Lionel Messi mwanasoka bora namba moja na Balotelli ni wa nne

    Pamoja na hayo, licha ya kuwa shabiki mkubwa wa Balotelli, Maradona anampa nafasi ya nne mshambuiaji huyo wa Milan katika orodha yake ya wachezaji bora duniani, akimuweka nyuma ya Lionel Messi, Cristiano Ronaldo na Neymar.
    Wakati huo huo, nyota huyo wa zamani wa Napoli amesema kwamba anapenda kurudi katika klabu hiyo kama kocha mara kocha wa sasa, Rafa Benitez atakapoondoka.
    Akiwa ameshinda mataji mawili ya Serie A na timu hiyo miaka ya 1987 na 1990, Nyota huyo wa Amerika Kusini amesema: "Wakati (Rafa) Benitez atakapoondoka ningependa kuikochi Napoli,".
    Napoli icon: The Italian side won the Serie A title in 1987 and 1990 with Maradona amongst their ranks
    Alama ya Napoli: Timu hiyo ya Italia ilishinda mataji ya Serie A mwaka 1987 na 1990 ikiongozwa na Maradona
    Hotseat: Former Liverpool and Chelsea boss Rafa Benitez (right) took charge of Italian side Napoli this summer
    Kitimoto: Kocha wa zamani wa Liverpool na Chelsea, Rafa Benitez (kulia) kwa sasa anaifundisha Napoli ya Italia aliyojiunga nayo msimu huu 

    Pamoja na hayo, mtu mzima huyo mwenye umri wa miaka 52 si rahisi sana kwake kupata nafasi hiyo: "Kuna mabadiliko ya makocha yanafanyika kila sehemu kutoka Hispania hadi Italy hadi England hadi Urusi, lakini watu fulani wananiogopa mimi. Ndiyo maana sikochi,."
    Maradona aliifundisha Argentina hadi kuifikisha Robo Fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2010 na kisha akaenda Dubai kufundisha klabu ya Al Wasl kwa msimu mmoja.
    Making the point: Having managed Argentina at the 2010 World Cup (below), Maradona claims he is not coaching at present as some people are 'afraid' of him
    Anatoa pointi: Akiwa ameifundisha Argentina katika Fainali za Kombe la Dunia 2010 (chini), Maradona amesema hafundishi kwa sasa kwa sababu watu fulani wanamuogopa
    Diego Maradona
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MARADONA ASEMA BAADA YA MESSI, RONALDO NA NEYMAR ANAYEFUATIA KWA UBORA DUNIANI NI BALOTELLI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top