KLABU ya Manchester United iko tayari kufufua mpango wa kumsajili 'Xavi mpya wa soka ya Hispania' ifikapo Januari kwa kumsajili kiungo wa Atletico Madrid, Koke.
Kinda huyo wa umri wa miaka 21 alikuwa kwenye rada za kocha wa zamani wa United, Sir Alex Ferguson msimu uliopita baada ya kufanya vizuri katika safu ya kiungo ya Atletico.
Ameendeleza makali hayo hata msimu huu, akiiwezesha Atletico kuwa nafasi ya pili katika ligi ya Hispania, La Liga nyuma ya Barcelona na pia kuingia katika timu ya taifa ya wakubwa ya Hispania.
Kivutio: Koke ni moyo ya safu ya kiungo ya Atletico
Lakini klabu ya Old Trafford, itarajie upinzani kutoka Nou Camp, ambako Barcelona bado wanamuwinda nyota huyo wa Atletico, pamoja na Real Madrid.
Koke kwa sasa anaweza kuuzwa kwa dau la Pauni Milioni 16 au zaidi na katika mbio za kuwania saini yake ni United na Barcelona ndio wako mstari wa mbele.
Nyota anayeibuka: Koke ameanza kuitwa kikosi cha wakubwa cha Hispania
0 comments:
Post a Comment