BAO la kujifunga la Inigo Martinez mapema dakika ya pili limetosha kuipa Manchester United ushindi wa 1-0 dhidi ya Real Sociedad Uwanja wa Old Trafford usiku huu na kupanda kileleni mwa Kundi A katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Martinez alijibabatiza mpira na kuudondoshea kwenye nyavu za timu yake sekunde ya 69 katika jitihada za kuokoa mpira uliopigwa Wayne Rooney.
United inapanda kileleni baada ya Shakhtar kufungwa 4-0 na Bayer Leverkusen ikitimiza pointi saba baada ya mechi tatu.
Kikosi cha Man Utd: De Gea, Rafael/Smalling dk59, Jones, Evans, Evra, Valencia, Carrick, Giggs, Kagawa, Hernandez/Young dk80 na Rooney.
Real Sociedad: Bravo, Carlos Martinez, Mikel Gonzalez, Martinez, De la Bella, Vela, Zurutuza/Castro dk75, Markel, Prieto/Pardo dk68, Griezmann na Seferovic/Agirretxe dk75.
Katika mechi nyingine zilizochezwa usiku huu, CSKA Moskva imelala 2-1 mbele ya Manchester City. Mabao ya City yalifungwa na Sergio Aguero dakika za 34 na 42, yote pasi za Negredo, wakati bao la wenyeji lilifungwa na Tosic dakika ya 32, pasi ya Honda.
Mabao mawili ya Cristiano Ronaldo dakika ya nne na 29 yameipa Real Madrid ushindi wa 2 - 1 dhidi ya Juventus, ambayo bao lake lilifungwa na Llorente dakika ya 22.
Galatasaray imeifumua mabao 3 - 1 Kobenhavn, mabao yake yakifungwa na Felipe Melo dakika ya 10, Wesley Sneijder dakika ya 38 na Didier Drogba dakika ya 45, wakati bao pekee la wapinzani wao limefungwa na Claudemir dakika ya 88.
Anderlecht imefungwa nyumbani 5-0 na PSG, Zlatan Ibrahimovic akifunga mabao manne dakika za 17, 22, 36 na 62, lingine likifungwa na Cavani dakikya 51, wakati Benfica imelazimishwa sare ya 1 - 1 nyumbani na Olympiakos Piraeus.
Mabingwa watetezi, Bayern Munich wameendeleza umwamba, baada ya kuifumua Viktoria Plzen 5-0, mabao ya Ribery dakika ya 25 na 61, Alaba dakika ya 37, Schweinsteiger dakika ya 64 na Gotze dakika ya 90.
Mistake: Inigo Martinez's early own goal gave Manchester United a perfect start at Old Trafford
Rebound: Wayne Rooney's original shot hit the post before Martinez put the rebound into his own net
Joy: Javier Hernandez, Ryan Giggs and Rooney celebrate the opening goal
Ruled out: Hernandez had a goal disallowed for offside during the first half
Pensive: Manchester United manager David Moyes shouts some instructions from the sidelines
Familiar face: Former United boss Sir Alex Ferguson was in the stands at Old Trafford
Loud: United trialled a new singing section to increase the atmosphere at Old Trafford
Back on track: Manchester City bounced back from their defeat by Bayern Munich with victory in Moscow
Triple threat: Paris Saint-Germain's Zlatan Ibrahimovic, centre, celebrates his hat-trick against Anderlecht
Man of the moment: Ibrahimovic celebrates scoring
In a league of his own: Cristiano Ronaldo scored twice for Real as they beat Juventus
Spot on: Ronaldo scores from a penalty
In it goes: Ronaldo beats Juventus goalkeeper Gianluigi Buffon from 12 yards
Battle in the air: Sergio Ramos vies with Juventus forward Carlos Tevez
Outnumbered: Andrea Pirlo is stuck between Real Madrid's Luka Modric and Karim Benzema
Leveling up: Fernando Llorente celebrates making it 1-1
Jumping for joy: Llorente celebrates with teammate Chiellini
High ball: Paul Pogba challenges for the ball with Real goalkeeper Iker Casillas
At the double: Ronaldo celebrates scoring his side's second goal
Floored: Ronaldo reacts after being fouled by Juventus' Giorgio Chiellini
Off you go: Giorgio Chiellini is sent off for his foul on Ronaldo
0 comments:
Post a Comment