KILA wiki wachambuzi Televisheni ya Japan wanamulika Old Trafford kuona Shinji Kagawa ataanzishwa katika kikosi cha kwanza cha Manchester United.
Kiasi cha nusu saa kabla ya mechi kuanza ni kawaida kufuatilia na sura zao hubadilika na kubeba hasira baada ya kuona hayumo katika kikosi cha kwanza.
Jumatano usiku ilikuwa tofauti, walipoonekana wenye sura za furaha baada ya Kagawa kuanza Manchester United. Jji la Tokyo lilihamia kwenye mchezo huo.
Alikuwemo kwenye kikosi kilichoanza dhidi ya Real Sociedad katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, akichezeshwa upande wa kushoto katika mechi yake ya nne kuanzishwa msimu huu.
Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Japan anafaa zaidi kucheza nambari 10 nyuma ya mshambuliaji mkuu, lakini anaweza kucheza popote kwa sasa.
Ilikuwa ni nafasi yake ya kung'ara katika mchezo mkubwa wa Ligi ya Mabingwa; kwa kuanzishwa tangu mwanzo wa mchezo. Alitua United kifalme baada ya kung'ara akiwa na Borussia Dortmund, lakini amejikuta katika wakati mgumu kuendana na mchezo wa kutumia miguvu wa soka wa England.
Kagawa alichezeshwa winga lakini hakufanya vizuri
Pembeni: Kagawa alichezeshwa winga
Koha David Moyes anataka mchezaji mwenye kasi; mchezaji mpiganaji ambaye anaweza kutambuka kwanza na kutoa pasi nzuri kwa Wayne Rooney. Namna hiyo.
Kagawa ni mchezaji laini, ambaye kwa sasa hawezi kumshawishi Moyes kumpa nafasi.
Anaingia katika msimu wa pili United, akipambana kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza, lakini bado anakabiliwa na kibarua kigumu na Jumamosi katika mchezo na Stoke anatarajiwa kurudi benchi tena.
Kagawa anataka kucheza katika nafasi ya Rooney, lakini hafikii ubora wa mpinzani wake katika nafasi hiyo. Rooney alikuwa vizuri.
Kagawa anabaki kuwa mchezaji chaguo la kwanza wa akiba kwa Rooney.Ni orodha ndefu ya mawinga bora waliowahi kung'ara United, kama George Best, Steve Coppell, Andrei Kanchelskis na Ryan Giggs na kwa bahati mbaya Kagawa hawakaribii kabisa
Siyo nafasi yake: Kagawa anafaa kucheza namba 10, lakini Wayne Rooney ni chaguo la kwanza huko
Yuko juu: Wayne Rooney alikuwa akihaha Uwanja mzima
0 comments:
Post a Comment