// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MAN UNITED, CHELSEA WALIE TU, LEWANDOWSKI AMEKWISHAMALIZANA NA BAYERN NA ATAPEWA PAUNI MILIONI 10 KUSAINI TU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MAN UNITED, CHELSEA WALIE TU, LEWANDOWSKI AMEKWISHAMALIZANA NA BAYERN NA ATAPEWA PAUNI MILIONI 10 KUSAINI TU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, October 18, 2013

    MAN UNITED, CHELSEA WALIE TU, LEWANDOWSKI AMEKWISHAMALIZANA NA BAYERN NA ATAPEWA PAUNI MILIONI 10 KUSAINI TU

    MSHAMBULIAJI Robert Lewandowski atapokea dau la usajili la karibu Pauni Milioni 10 atakapojiunga na Bayern Munich kama mchezaji huru mwishoni mwa msimu.
    Mabosi wa Allianz Arena wamepuuzia madai kwamba mshambuliaji huyo wa Borussia Dortmund ana fikra mbadala juu ya kujiunga na Bayern na wamesistiza watamalizana naye wakati wa mwaka mpya.
    Haruhusiwi kuingia kwenye mazungumzo rasmi na timu oyote hadi wakati huo, lakini BIN ZUBEIRY inafahamu kumekuwa na mbinu za ujandanda ambazo zimefanikisha makubaliano ya Mkataba wa miaka minne, ambao yeye atapewa dau la kumwaga wino la Pauni Milioni 9 na mshahara wa Pauni 150,000 kwa wiki.

    Anahama: Robert Lewandowski amefikia makubaliano ya kupewa karibu Pauni Milioni 10 za dau la usajili na Bayern
    Uthibitisho wa kuhamia kwake Bayern ni pigo kwa klabu za Manchester United na Chelsea, ambao walikuwa na matumaini ya kumnasa na kuwapiku mabingwa wa Bundesliga, kufuatia maelezo yake wakati wa maandalizi ya mchezo wa timu yake ya taifa, Poland dhidi ya England uliopigwa Uwanja wa Wembley Jumatano usiku.
    Alipoulizwa kuhusu mustakabali wake, alisema: "Nitakuwa tayari kusaini Mkataba na klabu yoyote Januari, lakini sijawahi kusema nitasaini Mkataba na Bayern. Siku moja, ningependa kucheza Ligi Kuu (England). Itakuwa uzoefu babu kubwa,".
    Heading to Munich? Lewandowski looks set to leave Borussia Dortmund on a Bosman
    Anakwenda Munich? Lewandowski anaonekana kujiandaa kuondoka Borussia Dortmund kutua Bosman
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAN UNITED, CHELSEA WALIE TU, LEWANDOWSKI AMEKWISHAMALIZANA NA BAYERN NA ATAPEWA PAUNI MILIONI 10 KUSAINI TU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top