Polisi wakimsombasomba shabiki wa Simba baada ya kutokea vurugu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom TanzaniaBara baina ya timu hiyo na wageni Kagera Sugar ya Bukoba. Polisi walilazimika kurusha mabomu ya machozi kuwadhibiti mashabiki wa Simba SC waliokuwa wakivunja viti na kurusha uwanjani kwa kilichoonekana kukerwa na refa wa mchezo huo, Mohamed Theofile kuongeza dakika nne baada ya kutimia dakika 90 za kawaida, ambazo Kagera Sugar walizitumia kusawazisha bao na kupata sare ya 1-1. |
0 comments:
Post a Comment