NYOTA wa Manchester City, Yaya Toure amekaribishwa kwa mazungumzo na Mkuu wa Idara ya Vita dhidi ya Ubaguzi ya FIFA juu ya maoni aliyoyatoa kwa ajili ya kuwalinda wanasoka weusi katika Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018.
Jeffrey Webb, anayeongoza Idara hiyo ya bodi hiyo ya soka duniani, amethibitisha jana usiku kwamba anatarajia kukuta na kiungo wa Ivory Coast, Toure wakati City itakapokwenda kumenyana na Chelsea.
Webb, Makamu wa Rais wa FIFA alisema: "Nitakwenda katika mechi hiyo, hivyo natumai nitapata nafasi ya kuonana na Yaya. Nimeomba kuonana naye,".
Showdown: Yaya Toure is set to meet with FIFA for talks after he threatened to boycott the 2018 World Cup
CSKA Moscow walikanusha kwamba mashabiki wao walimlenga moja kwa moja Toure katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini UEFA, sheria za soka Ulaya, limeanza taratibu za kuchukua hatua za kinidhamu kwa tukio hilo la Jumatano.
Webb, ambaye ni Rais wa CONCACAF, amesita kuchukua hatua yoyote kwa CSKA au wenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018, Urusi akisema: "Nataka kujua Yaya alifikiri nini na kuisikia stori yake kwa undani."alisema Webb ambaye inafahamika atakwenda kukutana na Maofisa wa Urusi kuzungumza nao mjini Moscow.
Shocking: Toure was racially abused during City's Champions League game against CSKA Moscow
Piara Power, Mkurugenzi Mkuu wa kundi la vita dhidi ya uvaguzi Ulaya, FARE na Mjumbe wa Kamati ya Webb ya vita dhidi ya tatizo hilo alisema: "Hii inaonyesha kwamba kile anachowaza Yaya kimesikilizwa na hana sababu ya kuendelea kuumiza kichwa chake,".
0 comments:
Post a Comment