// Disable text selection (not fully reliable)
function disableSelection(element) {
element.setAttribute('unselectable', 'on');
element.style.userSelect = 'none';
element.style.MozUserSelect = 'none';
element.style.webkitUserSelect = 'none';
}
// Apply to the entire document body
document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() {
disableSelection(document.body);
});
MABINTI WA KIBONGO WAWAFUMUA MSUMBIJI 10-0 TAIFA JIONI HII - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINEMABINTI WA KIBONGO WAWAFUMUA MSUMBIJI 10-0 TAIFA JIONI HII - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
MABINTI WA KIBONGO WAWAFUMUA MSUMBIJI 10-0 TAIFA JIONI HII
Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam TIMU ya soka ya taifa ya wanawake kwa vijana chini ya umri wa miaka 20, The Tanzanites imeifunga Msumbiji mabao 10-0 katika mechi ya kwanza ya raundi ya Kwanza ya Kombe la Dunia kwa mabinti wa umri huo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni ya leo. Katika mchezo huo uliohudhuria na mashabiki wachache mno, hadi mapumziko, tayari Tanzanites walikuwa mbele kwa mabao 5-0.
Neema Paul kushoto akishangilia na Theresa Yona baada ya kuifungia bao la kwanza Tanzania katika ushindi wa 10-0 jioni hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Bao la kwanza lilifungwa dakika ya sita na Neema Paul aliyeunganisha pasi ya Theresa Yona, kutoka wingi ya kushoto, wakati mfungaji bora wa michuano ya kimataifa ya Airtel Rising Stars iliyofanyika mwaka huu Nigeria, Shelder Boniface alifunga la pili dakika ya 24 baada ya kupangua ngome na kumpiga chenga hadi kipa. Deonesia Daniel akafunga bao la tatu kwa shuti kali la mpira wa adhabu lililotinga moja kwa moja nyavuni dakika ya 32 na dakika ya 41, Amina Ali akafunga la nne kwa shuti kali kutoka nje ya eneo la mita 18.
Wachezaji wa Tanzania wakishangilia mabao 10-0
Shelder Boniface akichezewa rafu na beki wa Msumbiji, Esperanca Malaita
Winga wa Tanzania, Theresa Yona akimtoka beki wa Msumbiji, Esperanca Malaita
Theresa amepiga krosi
Shelder Boniface alifunga bao tamu sana, akipiga chenga mabeki watatu na kipa wao
Shelider Boniface alifunga bao ambalo lingekuwa la tano dakika ya 45, lakini refa Ines Niyonsara wa Burundi akakataa. Kipindi cha pili The Tanzanites inayofundishwa na Rogasian Kaijage ilirudi na moto wake na kufanikiwa kupata bao tano, mfungaji Neema Paul aliyeunganisha krosi ya Theresa Yona. Hatimaye Shelder alifunga bao la sita dakika ya 80 akimalizia mpira uliotemwa na kipa kufuatia shuti la Stumai Abdallah. Dakika ya 82 Tanzania ikapata bao saba kupitia kwa Amina Ali aliyefumua shuti kutoka katikati ya Uwanja.
Kiungo wa Tanzania, Amina Ali akipambana na kiungo wa Msumbiji, Deolinda Gove
Theresa Yona alikuwa mwiba mkali leo kwa Msumbiji
Amina Ali akiwaonyesha kazi wachezaji wa Msumbiji
Kikosi cha Msumbiji leo
Kikosi cha Tanzania leo
Mashabiki wakiisapoti timu ya Tanzania leo
Tanzanites walipata bao la nane dakika ya 86 kupitia kwa Deonesia Daniel aliyefunga kwa mkwaju wa penalti, baada ya Shelder Boniface kuangushwa kwenye eneo la hatari. Dakika ya 89 Tanzania ilipata bao tisa kupitia kwa Amina Ali tena, ambaye alikuwa nyota wa mchezo huo. Stumai Abdallah akaifungia Tanzania bao la 10 dakika ya 90. Kikosi cha Tanzania kilikuwa; Celina Julius, Stumai Abdallah, Maimuna Said/Amina Hebron dk60, Fatuma Issa, Anastazia Anthony, Deonisia Daniel, Vumilia Maarifa, Amina Ali, Neema Paul, Shlder Boniface na Theresa Yona. Msumbiji; Paulina Jambo/Catarina Francue dk50, Esperanca Malaita/Delice Assane dk52, Felismisa Moiane, Emma Paulino, Gilda Macamo, Deolinda Gove, Jessica Zunguene, Cidalia Cuta, Nelia Magate, LonicaTsanwane na Onesema David.
Lookman crowned African footballer of the year
-
The 2024 Confederation of African Football (CAF) Award took center stage on
Monday night, with the best talents in African football emerging winners.
The...
Edozie Njoku and the new APGA
-
By Ambrose Ododo it has been a long and tortuous journey for the birth of
the rebranded All Progressives Grand Alliance, APGA, and it looks like it
is go...
Reports: Jack Wilshere set for Arsenal return
-
Former Arsenal midfielder Jack Wilshere has held talks with the north
London side on one of its vacant academy coaching roles. Under 23 manager
Per Mertes...
YANGA ‘KUPAA’ JUMANNE KUIFUATA MWADUI FC
-
MARA baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Namungo Fc kwenye uwanja wa
Majaliwa, Lindi, siku ya jumapili, Kikosi cha Young Africans Sports Club,
kitareje...
0 comments:
Post a Comment