IMEWEKWA OKTOBA 1, 2013 SAA 7:07 USIKU
MSHAMBULIAJI Romelu Lukaku amefunga mabao mawili katika ushindi wa 3-2 wa Everton usiku huu dhidi ya Newcastle United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England uliofanyika Uwanja wa Goodison Park.
Lukaku alifunga mabao hayo katika dakika za tano na 37,wakati lingine lilifungwa na Barkley dakika ya 25 na mabao ya Newcastle United yalifungwa na Cabaye dakika ya 51 na Remy dakika ya 89.
Mshambuliaji huyo anamuonyesha kocha wa Chelsea, Mreno Jose Mourinho kwamba alikosea kumruhusu kuondoka majira ya joto.
Kikosi cha Everton kilikuwa; Howard, Baines, Distin, Jagielka, Coleman, Mirallas/Deulofeu dk73, McCarthy, Barry, Osman/Stones dk90, Barkley/Naismith dk88 na Lukaku.
Newcastle United: Krul, Debuchy, Yanga-Mbiwa/Williamson dk45, Coloccini, Santon, Anita/Cisse dk69, Tiote, Sissoko, Gouffran, Remy na Ben Arfa/Cabaye dk45.
Mtu hatari: Romelu Lukaku ameifungia mabao mawili Everton ikiilaza Newcastle 3-2 Uwanja wa Goodison Park
Dakika tano zilitosha kwa Lukaku kufunga bao la kwanza
Barkley akishangilia baada ya kufunga
Lukaku akifunga bao la kwanza
Lukaku akifunga bao lake la pili