Boniface Wambura, IMEWEKWA OKTOBA 1, 2013 SAA 9:27 ALASIRI
LIPULI, MAJIMAJI KUUMANA WAMBI FDL
MECHI ya Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara (FDL) kati ya Lipuli ya Iringa na Majimaji ya Songea sasa itachezwa kesho (Oktoba 2 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Wambi uliopo Mafinga badala ya Uwanja wa Kumbukumbu ya Samora mjini Iringa.
Mabadiliko hayo yamefanyika kutokana na Serikali kuutumia Uwanja wa Kumbukumbu ya Samora kwa ajili ya shughuli za mbio za Mwenge.
Mechi nyingine ya FDL kesho itakuwa kati ya Tessema FC ya Dar es Salaam na Ndanda FC ya Mtwara, na itafanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam.
Lipuli imekimbiwa na kocha wake, Nahodha wa zamani wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Nsajigwa Shadrack aliyedai masharti yamezidi katika timu hiyo. Lipuli ilikuwa timu ya kwanza Nsajigwa kufundisha baada ya kustaafu akiwa na klabu ya Yanga msimu uliopita.
Wakati huo huo; walalamikiwa waliofikishwa kwenye Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wakiwa wameshapokea uamuzi dhidi yao kwa maandishi, mwisho wa kukata rufani Kamati ya Rufani ya Maadili ni kesho (Oktoba 2 mwaka huu).
Walalamikiwa wote saba waliohudhuriwa mashauli dhidi yao; Kamwanga Tambwe, Nazarius Kilungeja, Omar Abdulkadir, Richard Rukambura, Riziki Majala, Shaffih Dauda na Wilfred Kidao wamepokea uamuzi wa Kamati hiyo inayoongozwa na Jessie Mnguto.
Kwa mujibu wa Kanuni za Maadili, kwa ambao hawakuridhika na uamuzi huo wanatakiwa kukata rufani Kamati ya Rufani ya Maadili inayoongozwa na Jaji Mstaafu Stephen Ihema ndani ya siku tatu zinazomalizika kesho.
Rufani ziwasilishwe kwa Katibu Mkuu wa TFF kabla ya saa 10 kamili jioni. Kwa mujibu wa Kanuni ya 74 (1) na (2) ya Kanuni za Maadili, rufani zikionesha sababu za kufanya hivyo zinatakiwa kuwasilishwa ndani ya siku tatu kwa njia ya posta (registered post or dispatch or courier service) kwa Sekretarieti.
Vilevile inatakiwa rufani inatakiwa kuambatanishwa risiti ya malipo ya ada ya rufani. Ada ya rufani ni sh. milioni moja.

Bosi; Nsajigwa Shadrack sasa ni kocha wa Lipuli |