MSHAMBULIAJI Robert Lewandowski amezipa nafasi klabu za Manchester United, Manchester City na Chelsea za England kugombea saini yake, baada ya kusema ameghairi kwenda Bayern Munich.
Mpachika mabao huyo wa Poland, ambaye anatarajiwa kucheza dhidi ya England Uwanja wa Wembley leo, alifikiriwa atajiunga na mabingwa hao wa Ulaya kama mchezaji huru msimu ujao.
Lakini nyota huyo wa Borussia Dortmund amekanusha kufikia makubaliano ya kusaini Mkataba na Bayern na amesema angependa kuchezea klabu moja kubwa ya England.
Atahamia Ligi Kuu England? Mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Robert Lewandowski (kushoto) amekanusha kuwa na mpango wa kuhamia Bayern Munich
Mshambuliaji wa nguvu: Lewandowski (kulia), akipambana na Edmar Holovsky wa Ukraine
"Nitakuwa tayari kusaini Mkataba (na klabu yoyote) ifikapo Januari, lakini sijawahi kusema kwamba nitasaini mkataba na Bayern," alisema Lewandowski, mwenye umri wa miaka 25.
"Yalikuwa ni maelewano mabaya. Ni kweli nilipata nafasi ya kuzungumza Sir Alex Ferguson (mwaka jana), lakini hatukuzungumzia usajili. "Siku moja ningependa kucheza Ligi Kuu England. Nitakuwa na uzoefu mkubwa.'
Mkataba wa Lewandowski katika klabu yake, Dortmund unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu na klabu zote za Manchester na Chelsea zimekuwa zikimmezea mate mkali huyo wa mabao kwa muda sasa.
Mkali wa mabao: Lewandowski (kushoto) amekuwa mmoja wa washambuliaji tishio Ulaya baada ya kuisaidia Borussia Dortmund kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu uliopita
Leo Wembley tena: Lewandowski aliondoka na maumivu mara ya mwisho alipocheza Uwanja wa Wembley baada ya Borussia Dortmund kufungwa na Bayern Munich katika Fainali ya Ligi ya Mabignwa
0 comments:
Post a Comment